Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-SIASA

Zuma kulihutubia taifa Bungeni chini ya ulinzi mkali

Spika wa bunge la kitaifa nchini Afrika Kusini, Baleka Mbete, amesema kuwa, agizo la rais Jacob Zuma la kupeleka wanajeshi zaidi ya 400 kwenye viunga vya bunge, halitaathiri shughuli za bunge hilo wakati rais Zuma atakapokuwa akitoa hotuba yake kwa taifa hii leo.

Rais Jacob Zuma atazamiwa kutoa hotuba yake kwa taifa la Afrika Kusini Alhamisi Februari 9.
Rais Jacob Zuma atazamiwa kutoa hotuba yake kwa taifa la Afrika Kusini Alhamisi Februari 9. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Spika Mbete amelazimika kutoa kauli hii, baada ya hatua ya rais Zuma kukosolewa vikali, huku bunge likituhumiwa kuruhusu kuingiliwa kwa madaraka yake hasa kwenye masuala ya ulinzi, kwa hofu kuwa huenda kukatokea vurugu bungeni.

Mara kadhaa wakati wa hotuba kama hii, wabunge wa upinzani wamekuwa wakifanya fujo kupinga hotuba hiyo kutolewa na rais Zuma wakimtuhumu kwa kukiuka katiba, makabiliano ambayo husababisha kutumiwa nguvu kuwaondoa bungeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.