Pata taarifa kuu
GAMBIA-ICC-BARROW-HAKI

Adama Barrow: Gambia haitojiondoa ICC

Rais wa Gambia Adama Barrow, ameelezea ahadi ya kampeni yake ya kutokubali nchi yake kujiondoa katika mkataba wa Roma ulioanzisha Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) na kubaini kwamba nchi yake itasalia kuwa mwanachama wa mahakama hiyo.

Rais wa Gambia Adama Barrow asema Gambia bado ni mwanachama wa ICC
Rais wa Gambia Adama Barrow asema Gambia bado ni mwanachama wa ICC REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Rais Barrow amefuta uamuzi wa mtangulizi wake, Yahya Jammeh, ambaye alikuwa aliitaja ICC kama "mahakama ya kimataifa kwa ajili ya mateso na udhalilishaji wa watu weusi, hasa Waafrika".

Rais wa Gambia ametoa tangazo hilo kufuatia mkutano na Neven Mimica, Kamishna wa Umoja wa Ulaya kwa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo, mjini Banjul.

Adama Barrow alishinda uchaguzi wa urais mwezi Desemba kwa ahadi ya kutetea haki za binadamu na uhuru.

Ujio wake umemaliza utawala wa Yahya Jammeh ambaye aliongoza nchi ya Gambia kwa mkono wa chuma kwa miaka 22.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.