Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI-KIFO

Mazungumzo yaendelea kuhusu mazishi ya Etienne Tshisekedi

Tume ya serikali ililikutana kwa mara ya kwanza na ujumbe kutoka familia ya Etienne Tshisekedi na chama cha UDPS Jumatatu hii, Januari 6, kwa ajili ya mazishi ya kiongozi wa kihistoria wa upinzani nchini DR Congo. Hakuna mpango rasmi ambao umetangazwa ikiwa ni pamoja na kurejeshwa kwa mwili wa mwanasiasa huyo wala kwa mazishi yake.

Jeneza la Etienne Tshisekedi likiwa chini ya ulinzi mkali katika mji wa Brussels, Januari 5, 2017.
Jeneza la Etienne Tshisekedi likiwa chini ya ulinzi mkali katika mji wa Brussels, Januari 5, 2017. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Wadadisi wanaona kuwa tukio hili huenda likawa la kisiasa, licha ya kuwa maelfu ya wananchi wa Dr Congo wanataka kuhudhuria mazishi hayo.

Askofu wa Mweka, Gerard Mulumba, ndugu wa Etienne Tshisekedi aliongoza ujumbe wa familia. Chama cha UDPS, Etienne Tshisekedi akiwa ni mmoja wa waanzilishi wa chama hicho, kiliwakilishwa pia na mmoja wa Makatibu wake Wakuu. Tume ya serikali kwa upande wake, iliongozwa na Emmanuel Ramazani Shadary, Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani. hata hivyo inaonekana kuwa mazishi ya Etienne Tshisekedi huenda yakazua hali ya sintofahamu katika suala la salama na vifaa, chanzo cha usalama kimesema.

Ujumbe wa watu kumi na tano, ikiwa ni pamoja na familia yake hasa wanasiasa kutoka chama chake, wanatarajiwakwenda mjini Brussels wiki hii ili kutatua masuala ya mwisho yanayohusiana nakurejeshwa kwa mwili wa mwanasiasa huyo mkongwe. Miongoni mwa fikra zilizojadiliwa kwa ajili ya mazishi mjini Kinshasa, ni pamoja na mazishi ya kiserikali katika sehemu ya majengo a Bunge. Hata hivyo kulikuwa kumepangwa kwamba zoezi la kuuwaga mwili wa Etienne Tshisekedi lifanyike katika uwanja wa Martyr, ambao ni uwanja mkubwa katika mji wa Kinshasa.

Lakini chama pia kinafikiria kujenga sanamu la kiongozi huyo wa upinzani. mradi ambao unaweza kuchukua muda mrefu.

Maelfu ya raia wa Dr Congo waishio ugenini wakitoa heshima za mwisho kwa kiongozi mkuu wa upinzani Etienne Tshisekedi, Februari 5, 2017.
Maelfu ya raia wa Dr Congo waishio ugenini wakitoa heshima za mwisho kwa kiongozi mkuu wa upinzani Etienne Tshisekedi, Februari 5, 2017. REUTERS/Francois Lenoir

Itafahamika kwamba wanasiasa wa chama cha UDPS, lakini pia wale kutoka muungano wa Rassemblement walidai mwishoni mwa wiki hii kwamba waziri mkuu mpya aliyechaguliwa na chama cha UDPS aweze kuteuliwa kabla ya mazishi. Au Waziri Mkuu wa sasa, afutwe kazi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.