Pata taarifa kuu
MALI

Rais wa Mali atoa wito wa kusahihisha mapungufu ya Minusma

Rais wa Mali ametoa wito wa kusahihisha mapungufu ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma) wakati wa sherehe za ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za G5 Sahel.

Rais wa Mali  Ibrahim Boubacar Keïta, Septemba 9, 2013, mjini Bamako.
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta, Septemba 9, 2013, mjini Bamako. AFP PHOTO / HABIBOU KOUYATE
Matangazo ya kibiashara

Marais wa Burkina Faso, Mauritania, Niger na Chad wanahudhuria mkutano huo, ulioitishwa kwa sababu ya kuzorota kwa hali ya usalama nchini Mali.

Shambulizi la hivi karibuni lilifanyika katika mji wa Menaka kaskazini mwa Mali ambapo askari wanne waliuawa Jumamosi.

Lakini shambulizi liliyosababisha hasara kubwa katika miaka ya hivi karibuni bado ni lile lililotokea katika mji wa Gao, ambapo karibu watu 80 waliuawa Januari 18.

Kuzorota kwa hali ya usalama nchini Mali kunasababisha nchi za ukanda huo kuwa katika hali ya hatari.

Niger na jirani yake Burkina Faso mara kwa mara zinakabiliwa na vitendo vya kigaidi ambapo inasemekana kwamba wahusika wa mashambulizi hayo wanatoka Mali au baada ya vitendo vya viovu hukimbilia nchini Mali.

Siku ya Jumapili Mawaziri Usalama, Ulinzi na Mambo ya Nje kutoka G5 Sahel walijadili kuhusu nakala itakayosilishwa kwa Marais.

Inasemekana kuwa kuna uwezekano wa kuundwa kwa kikosi cha ukanda ili kukabiliana na vitendo hivyo viovu.

Hakuna maelezo juu ya idadi ya askari na tarehe ya kuanzishwa kwa kikosi hicho.

Raia wa ukanda wa Sahel na hasa wananchi wa Mali wana matumaini zaidi na mkutano huo.

G5 Sahel inayoundwa na Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger na Chad ilianzishwa mwaka 2014. Ni mfumo wa uratibu na ushirikiano katika sera ya maendeleo na usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.