Pata taarifa kuu
LLIBYA-ITALIA-WAHAMIAJI

Mediterranean: wahamiaji 1,500 waokolewa mwishoni mwa wiki hii

Wahamiaji 1,500 wamrokolewa mwishoni mwa wiki hii katika pwani ya Libya, idadi ambayo ni kubwa katika msimu huu wa baridi ambapo idadi imepungua kutokana na hali ngumu ya hali ya hewa.

Mhamiaji mwanamke na mtoto waliokolewa na kikosi cha walinzi cha pwani ya Libya, wakiwasili Februari 5, 2017 mji wa Tripoli.
Mhamiaji mwanamke na mtoto waliokolewa na kikosi cha walinzi cha pwani ya Libya, wakiwasili Februari 5, 2017 mji wa Tripoli. AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi hii, iliotolewa na walinzi wa pwani ya Italia ambao wanaratibu shughuli katika eneo hilo, imefikia sasa zaidi ya wahamiaji 4,500 waliokolewa tangu siku ya Jumatano.

Siku ya Jumapili, wahamiaji 900 ambao walikua wakisafiri katika boti tatu wameokolewa katika bahari ya Mediterranean na meli ya kikosi cha jeshi la majini cha Uhispania (Canarias), na meli zingine za kawaida.

Siku moja kabla, wahamiaji 600waliookolewa bila tatizo lolote wakati wa shughuli tisa tofauti zilizoendeshwa na Diciotti, meli ya kikosi cha walinzi wa pwani ya Italia.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya waliokutana mjini Malta, waliahidi siku ya Ijumaa kusaidia nchi ya Libya kupambana dhidi ya wapita njia, lakini mashirika mengi ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali yalionya dhidi ya hatua zitakazochukuliwa.

Italia na Libya kwa upande wao, walisaini mkataba wa makubaliano unaoelezea uimarishaji wa mipaka yao ili kufanikisha, kwa msaada wa Umoja wa Ulaya, kupunguza wingi wa wahamiaji kutoka Afrika Kaskazini kuelekea nchini Italia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.