Pata taarifa kuu

Silaha zakamatwa nyumbani kwa Yahya Jammeh

Kikosi cha askari wa Jumuiya ya mataifa ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS waliotumwa nchini Gambia kimetangaza kwamba kimekamata silaha na vifaa vya kijeshi katika nyumba binafsi ya aliyekua rais wa Gambia Yahya Jammeh.

Yahya Jammeh mwenye vazi jeupe akiondoka mjini Banjul, kulia ni mlinzi wake akiwa analia. Januari 21, 2017
Yahya Jammeh mwenye vazi jeupe akiondoka mjini Banjul, kulia ni mlinzi wake akiwa analia. Januari 21, 2017 REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

“Silaha zote na vifaa vya kijeshi kwa sasa viko mikononi mwa ECOWAS. Hakuna kitu kitakachotokea huko kanilai. Hali ya usalama imedhibitiwa, “ Jenerali François Ndiaye, mkuu wa tume ya ECOWAS nchini Gambia (Micega) amehakikisha.

Kanilai, kijiji aklikozaliwa Yahya Jammeh, kinapatikana magharibi mwa Gambia, karibu kilomita 100 mashariki mwa mji mkuu wa Gambia, Banjul.

“Vikosi vya jeshi la Gambia vimeshirikiana vizuri na kikosi cha ECOWAS, Jenerali Ndiaye ameviambia vyombo vya habari, mjini Banjul.

Amekataa kuelezea idadi ya silaha zilizokamatwa.

Mkuu wa Micega, hata hivyo, amesema kuwa kiongozi wa kikosi cha ulinzi wa rais cha jeshi la Gambia Jenerali Bora Colley, amekamatwa katika nchi jirani ya Senegal.

Lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu kukamatwa kwa afisaa huyo wa jeshi la Gambia ambapo polisi ya Senegal litangaza kuwa ilimkamata toka siku nyingi zilizopita

Jenerali François pia Ndiaye amebaini kwamba askari wanne wa kikosi cha ulinzi wa mkee wa yahya jammeh wamekamatwa.

Kwa mujibu wa Jenerali François Ndiaye, walikua wakijaribu kurudi nchini Gambia baada ya kumshindikiza mkee wa Yahya Jammeh ukimbizini.

Askari hao waliokamatwa katika mji wa Karang, karibu na mpaka na Senegal, waliwekwa kizuizini siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Vikosi vya ECOWAS vilimshawishi Yahya Jammeh kuachia ngazi na kumkabidhi madaraka Adama barrow, aliyeshinda uchaguzi wa rais wa Desemba 1, 2016.

Bw Jammeh, madarakani tangu kwa muda wa miaka 22, alikua alikubali kushindwa kabla ya kubadili kauli na kusababisha mgogoro wa kisiasa nchini gambia, mgogoro ambao ulimalizika baada ya kuondoka na kupewa hifadhi nchini Equatorial Guinea jioni ya tarehe 21 Januari 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.