Pata taarifa kuu
AU-UONGOZI

Tume ya AU: Wagombea watano kumrithi Dlamini-Zuma

Watu watano wanawania katika kinyang'anyiro cha kuchukua nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. Mawaziri wa Mambo ya Njee kutoka nchi za Afrika wanakutana kuanzia Jumatano wiki hii hadi Ijumaa Januari 27. Mkutano wa Marais utafanyika Jumatatu hadi Jumanne wiki ijayo.

Siège de l'Union africaine à Addis Abeba, en Ethiopie.
Siège de l'Union africaine à Addis Abeba, en Ethiopie. RFI/Neidy Ribeiro
Matangazo ya kibiashara

Wagombea hao ni wanaume na wanawake wenye uzoefu. Wanataka kufanya Tume hii ya Umoja wa Afrika chombo kwa ajili ya mageuzi ya bara la Afrika kwa hadi mwaka 2063. Wakuu wa nchi watakaokutana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, mwishoni mwa mwezi huu watachukua uamuzi.

Wagombea watano ambao wanawania kwenye nafasi muhimu ya mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika wote wanaozoefu katika siasa za Afrika, huku kila mmoja akiungwa mkono na nchi za ukanda wanakotoka. Kwa mara ya kwanza, Desemba 9, Umoja wa Afrika uliandaa mjadala wa televisheni kwa kuruhusu wagombea kujitambulisha na hasa kuwasilisha mipango yao kuhusu masuala ya demokrasia, utawala wa sheria lakini pia kuhusu swala la uhuru wa kuingia na kutoka katika nchi mojawapo, kuendeleza wanawake na vijana au suala la ufadhili wa mipango ya Umoja wa Afrika. Tukio hilo lilitazamwa na watu wengi kwenye televisheni, lakini pia kwenye mitandao ya kijamii. Itakumbukwa kwamba uchaguzi huu uliahirishwa katika mkutano wa kilele uliopita wa Umoja wa Afrikamjini Kigali, nchini Rwanda, baada ya kukosekana kwa wagombea wa kuaminika.

Picha kwenye tovuti ya AU zikionyesha wagombea watano kwenye nafasi ya uenyekiti wa Tume ya Au: Pelonomi Venson Moitoi, Moussa Faki Mahamat, Agapito Mba Mokuy, Amina Mohamed Jibril na Abdoulaye Bathily (kutoka kusoto kwenda kulia).
Picha kwenye tovuti ya AU zikionyesha wagombea watano kwenye nafasi ya uenyekiti wa Tume ya Au: Pelonomi Venson Moitoi, Moussa Faki Mahamat, Agapito Mba Mokuy, Amina Mohamed Jibril na Abdoulaye Bathily (kutoka kusoto kwenda kulia). Union africaine

Amina Jibril Mohamed, mwenye umri wa miaka 55

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kenya, mwanadiplomasia huu na mwanasheria ni mgombea wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki (EAC). Mgombea huyo kutoka Kenya alizaliwa mwaka 1961 katika familia maskini, lakini alifanikiwa kkupitia masomo yake (ana shahada ya Chuo kikuu cha Oxford katika Uhusiano wa Kimataifa) na uzungumzaji kwake ulimpelekea kuteuliwa katika nafasi za juu serikalini nchini mwake Kenya, inayongozwa kwa sehemu kubwa na wanaume.

Waziri alifanya kampeni zake katika masuala ya kiuchumi na kibiashara. Anapendekeza, iwapo atachaguliwa, kuifanya Afrika moja ya mipango yake muhimu katika uwekezaji wa kigeni."

Pelonomi Venson Moitoi, mwenye umri wa miaka 65

Pelonomi Venson Moitoi, pia, ni Waziri, hasa wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana. Mgombea aliyeshindwa mjini Kigali, Raia wa Botswana anajiamini kushinda kwenye nafasi hiyo na kuamua kuwania. Serikali ya Gaborone imejitahidi kuhamasisha kuhusu mgombea kwake kwa nchi zote za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ambao wanaamini katika mantiki ya mzunguko wa kikanda, uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika unarudi kwa mara nyingine tena kwa nchi ya ukanda wa kusini, ambapo Mwenyekiti wa sasa amefanya muhula mmoja pekee.

Bi Moitoi amezaliwa mwaka 1951 na ana shahada ya MBA ya Chuo Kikuu cha Central Michigan nchini Marekani. Waziri Mara kadhaa katika nchi yake. Kabla ya kuwa Waziri wa mambo ya Nje, alikua Waziri wa Usafiri, wa Mawasiliano, wa Kazi, wa Sayansi na wa Elimu. Alifanya kampeni kuhusu uzoefu wake wa miongo minne katika nafasi za juu serikalini nchini Botswana.

Lakini katika uchaguzi uliopita, nchi nyingi zilijizuia kumpigaa kura, pengine kwa sababu ya serikali ya Gaborone mara nyingi ilitofautiana na Umoja wa Afrika, hasa kuhusiana na suala la kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)ambapo hati zinazotolewa ilionekana kuwa zinawadhalilisha sana viongozi wa Kiafrika.

Agapito Mba Mokuy, mwenye umri wa miaka 51

Waziri wa Equatorial Guinea, Agapito Mba Mokuy ana umi mdogo kati ya wagombea watano wa wanaowania kumrithi Mwenyekiti wa sasa wa Tume ya Umoja wa Afrika. Anazumgumza lugha tano za kimataifa.

Abdoulaye Bathily, mwenye umri wa miaka 69

Mwanasiasa na mwanadiplomasia, Abdoulaye Bathily ni mgombea wa Senegal na ECOWAS ambapoo nchi 15 zmemeahidi kumpigia kura. Pia ana uzoefu imara wa kimataifa. Mwezi Julai 2013, aliwahi kuwa Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa ujumbe wa taasisi ya Mission Umoja wa Mataifa kwa kwa Mali (Minusma), kabla ya kuteuliwa kuwa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UN kwa Afrika Kati.

Alizaliwa mwaka 1947, Profesa Bathily ni mwanahistoria.Alichangia katika kisiasa za senegal na alikua mara kadhaa mbunge na waziri katika tawala za imepokea naibu kadhaa na waziri chini ya urais wa marais wa zamani wa marais wa zamani wa Senegal Abdou Diouf na Abdoulaye Wade.

Moussa Faki Mahamat, mwenye umri wa miaka 56

Mwanasheria, Moussa Faki Mahamat ni Waziri wa mambo ya Nje wa Chad tangu mwaka 2008. Alizaliwa mwaka 1960. Alihudumu kwenye nafasi za juu katika serikali ya Chad kwa karibu miaka thelathini. Alikuwa Waziri Mkuu wa nchi yake kati ya mwaka 2003 na 2005.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.