Pata taarifa kuu

Mvutano waibuka katika chama tawala Tunisia

Chama tawalanchini Tunisia cha Nidaa Tounes kinakabiliwa na malumbano ya ndani kufuatia uamuzi wa kumfukuza kiongozi wake Hafedh Caid Essebsi, mtoto wa Rais Essebsi, uamuzi ambo umepingwa na baadhi ya wajumbe wa chama hicho.

Hafedh Caid Essebsi mkurugenzi mtendaji wa chamatawala nchini Tunisia cha Nidaa Tounes.
Hafedh Caid Essebsi mkurugenzi mtendaji wa chamatawala nchini Tunisia cha Nidaa Tounes. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linaonyesha hatua nyingine katika mfululizo wa vita vya uongozi vinvyokukumba cham acha Nidaa Tounes tangu kuchaguliwa kwa mwanzilishi wake Beji Caid Essebsi kuwa rais mwaka 2015. Mgawanyiko huu umekidhoofisha chama tawala nchini Tunisia chama ambacho kilishinda uchaguzi wa Wabunge mwaka 2014 kabla ya kupoteza nafasi ya juu kwa Bunge kwa faida ya chama cha Kislamu cha Ennahda. Mvutano huo haujapatiwa suluhu

Jumatatu jioni Januari 23, moja ya makambi mawili hasimu ilitangaza katika taarifa yake kumfukuza Hafedh Caid Essebsi, mkurugenzi mtendaji wa chama katika chama hicho. Tangazo hilo "halina thamani ya kisheria na haina maana," amejibu Bw caid Essebsi kwenye redio binafsi Shems FM. Amesema watu sita waliosaini kwenye tangazo hilo "walitengwa" baada ya "kuzungumza bila idhini yoyote kwa lengo la kudhoofisha chama."

Huu ni "ujanja wenye lengo la kuyumbisha chama" cha Nidaa Tounes, amelaani Mourad Dalech, mwakilishi wa mkuu wa chama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.