Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA

Bunge la Gambia laondoa hali ya tahadhari

Bunge la Gambia limeondoa hali ya tahadhari iliyowekwa wiki iliyopita, siku nne baada ya kuondoka nchini Gambia kwa Rais wa zamani Yahya Jammeh, ambaye alikimbilia uhamishoni Humamosi katika nchi ya Equatoria Guinea.

Askari wa ECOWASwapiga kambi mbele ya Ikulu ya rais mjini Banjul, nchini Gambia tarehe 23 Januari 2017.
Askari wa ECOWASwapiga kambi mbele ya Ikulu ya rais mjini Banjul, nchini Gambia tarehe 23 Januari 2017. RFI/Guillaume Thibault
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC katika mji wa Banjul, mwanachama wa chama tawala cha zamani aliomba radhi kwa kuunga mkono uamuzi huu ambao lengo pekee iliku kuwasaidia rais wa zamani kubaki madarakani.

Hii ni hatua nyingine ya kurejea kwa demokrasia katika nchi hii ya Afrika Magharibi baada ya zaidi ya mwezi mmoja nchi ya Gambia kukumbwa na mgogoro wa kisiasa baada ya uchaguzi. Rais Jammeh ambaye alikuwa amekubali kushindwa katika uchaguzi wa rais wa Desemba 1 alibadilisha uamuzi wake na kukataa matokeo ya uchaguzi.

Baada ya mashauriano mbalimbali na mazungumzo yalioendeshw na ECOWAS, Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, Yahya Jammeh aliondoka nchini siku ya Jumamosi kupewa hifadhi nchini Equatorial Guinea. Mrithi wake Adama Barrow, ambaye ni yuko Senegal kwa siku kadhaa aliapishwa katika mji wa Dakar.

mgogoro wa kisiasa nchini Gambia umesababisha kukimbia kwa maelfu ya raia. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR), angalau raia elfu sabini na sita walikimbilia nchini Senegal tangu mwezi Desemba mwaka jana. 8000 kati yao tayari wamerejea nyumbani, UNHCR imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.