Pata taarifa kuu

Operesheni ya kijeshi yasimamishwa Gambia, Jammeh apewa makataa ya mwisho

Baada ya kuvuka mpaka na kuingia nchini Gambia Alhamisi hii, Januari 19, askari wa nchi za magharibi za Afrika wamesimamisha operesheni yao kwa jaribio la mwisho la kumshawishi Yahya Jammeh. Leo Ijumaa Rais wa Guinea Alpha Conde anatazamiwa kufanya ziara nchi Gambia kwa minajili ya kumshawishi Yahya jammeh kuachia ngazi.

Wananchi wa Gambia washerehekea kuapishwa kwa Adama Barrow katika mitaa ya mji wa Banjul, Januari 19, 2017.
Wananchi wa Gambia washerehekea kuapishwa kwa Adama Barrow katika mitaa ya mji wa Banjul, Januari 19, 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

aribio la mwisho katika kumuelewesha Yahya Jammeh kuachia ngazi kwa amani litafanyika leo Ijumaa, Mwenyekiti wa Tume ya ECOWAS Alain Marcel de Souza ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dakar, nchini Senegal. "Profesa Alpha Conde wa Guinea aliombwa kwa mara ya mwisho kumshawishi Yahya Jammmeh kuachia ngazi kwa amani. atasafiri kuelekea Gambia, na ujumbe wa ECOWAS na Umoja wa Mataifa. "

Baada mwenzake wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, rais wa Guinea atafanya ziara kujaribu kumshawishi Yahya Jammeh kuachia madaraka. "Kama saa sita mchana, atakua bado hajakubali kuondoka nchini chini jitihada za Profesa Alpha Conde, askari wataingilia kijeshi na kumuondoa madarakani, " ameonya Marcel Alain de Souza.

Rais mpya wa Gambia, Adama Barrow aapishwa nchini Senegal

Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow, hatimaye aliapishwa rasmi kuwa rais wa nchi hiyo katika ofisi za ubalozi wa Gambia zilizoko jijini Dakar, Senegal, huku akitoa wito kwa wanajeshi kuonesha utii kwa Serikali yake.

Rais Barrow, amelazimika kuapishwa nje ya nchi yake kutokana na kuhofia usalama wake pamoja na hatua ya rais Yahya Jammeh kukataa kuondoka madarakani, akipinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka jana.

Awali kabla ya kuapishwa kwake, wizara ya mambo ya nje ya Senegal ilidai kuwa kiongozi huyo angeapishwa kwenye ardhi ya nchi yake, lakini haikuwa hivyo na sasa rais Barrow amekula kiapo cha utii kwa nchi yake kwenye ubalozi wa Gambia nchini Senegal.

Barrow toka kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais, ameungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa, lakini mpinzani wake Yahya Jammeh amekataa kuondoka madarakani, akitaka kwanza pingamizi lake la uchaguzi lisikilizwe na mahakama kuu iliyosema inauwezo wa kusikiliza shauri hilo mwezi Mei.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.