Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Watu 44 wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga Gao

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amewaua watu wasiopungua 44 ikiwa ni pamoja na waasi wa zamani na wapiganaji wa makundi wanaounga mkono serikali mjini Gao kwa kujilipua Jumatano hii, Januari 18 katika kambi yao kaskazini mwa Mali, kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi katika Umoja wa Mataifa.

Kwenye eneo la shambulio, Jumatano 18 Januari katika kambi ya jeshi mji wa Gao, nchini Mali.
Kwenye eneo la shambulio, Jumatano 18 Januari katika kambi ya jeshi mji wa Gao, nchini Mali. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulitokea mapema asubuhi Jumatano Januari 18 katika mjini Gao, mji mkuu wa kaskazini mwa Mali. Kwenye umbali wa mita 500 kutoka uwanja wa ndege, mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyekua katika gari aliingia kambini na kujilipuliwa. Mashahidi wanasema walisikia "mlipuko mkubwa". Taarifa hii imethibitishwa na kiongopzi mmoa tawala kutoka mji huo wa Mali, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Angalau watu 44 wameangamia katika mlipukohuo kulingana na ripoti ya muda ya serikali. Watu wengi waliojeruhiwa walisafirishwa katika hospitali ya mjini Gao na kulindwa na askari. Serikali ya Mali imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa. Waziri wa Ulinzi wa Mali pia anatarajiwa kutembelea eneo la tukio.

Shambulio hilo linatokea wiki mmoja baada ya rais wa Ufaransa Francois Hollande kuzuru kambi hiyo ya mjini Gao ambapo maelfu ya askari wa Ufaransa walikuwepo.

Wakati huo huo rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita amewataka wananchi wa Mali kushikamana na kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kukabiliana na mashambulizi kama hayo.

Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo, na polisi ya amli imeanzisha uchunguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.