Pata taarifa kuu
GAMBIA-SENEGAL-BARROW

Adama Barrow apewa ulinzi mkali nchini Senegal

Baada ya kuondoka nchini Gambia siku tatu zilizopita Adama Barrow aliyeshinda katika uchaguzi wa urais nchini Gambia, kwa sasa anaishi kwa muda nchini Senegal, kwa mujibu wa serikjali ya Senegal.

Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow, apewa makao nchini Senegal, hadi atakapotawazwa Januari 19, 2017.
Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow, apewa makao nchini Senegal, hadi atakapotawazwa Januari 19, 2017. REUTERS/ Thierry Gouegno
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa rais mteule wa Gambia Adama Barrow amesema, sherehe ya kumwapisha zitaendelea kama zilivyopangwa siku ya Alhamisi juma hilli jijini Bunjul.

Hakikisho hili linakuja wakati huu Barrow akiwa nchini jirani ya Senegal, atakakokuwa hadi kuapishwa kwake.

Hatua ya Barrow, kwenda Senegal ilishachukuliwa na viongozi wa Afrika Magharibi ECOWAS waliokutana nchini Mali mwishoni mwa juma, baada ya rais Yahya Jammeh kuendelea kukataa kuondoka madarakani.

Ripoti kutoka chini Senegal zinasema kuwa rais mteule wa Gambia Adama Barrow atasalia nchini Senegal hadi wakati wa kuapishwa kwake wakati huu ambapo nchi ya Gambia inakumbwa na mzozo wa kisiasa ulizuka baada ya rais Yahya Jammeh kukataa kuachia ngazi.

Vyombo vy habari nchini Senegal vimearifu kwamba rais wa Senegal Macky Sall, amekubali kumpa makao bwana Barrow katika mji mkuu Dakar hadi hadi Januari 19 siku ambayo atakapoapishwa na kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi ya Gambia.

Jumamosi Januari 14, rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, alimtaka rais wa Gambia kuachia ngazi ifikapo tarehe 19 Januari ili kuzuia umwagaji damu.

Rais Yahya Jammeh ameendelea kukataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Desemba na kusema bado anasubiri uamuzi wa mahakama ya juu kuhusu madai aliyowasilisha kwa mahakama hiyo, ambayo hivi karibuni iliahirish akusikiliza kesi hiyo hadi mwezi Mei mwaka 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.