Viongozi zaidi ya 40 wakutana katika mkutano wa 27 wa Africa na Ufaransa Bamako nchini Mali
Imechapishwa:
Cheza - 21:09
Makala hii inaangazia mkutano wa 27 wa viongozi zaidi ya 40 ambao wanakutana jumamosi hii kujadili maswala ya usalama na ya kijamii, mkutano ambao unaongozwa na rais wa Ufaransa Francois Hollande katika mji mkuu wa Mali, Bamako. Mkutano huu unafanyika wakati ambapo kuna hali ya wasiwasi nchini humo kufuatia kuwepo kwa makundi kadhaa ya wapiganaji wenye kushirikiana na magaidi katika eneo hilo. Pia tumeangazia hali iliyojiri wiki hii huko Burundi, DRC, Gambia, Rwanda, Uganda na maadhimisho ya miaka 53 ya mapinduzi visiwani Zanzibar, wakati kimataifa kauli ya katibu mkuu mpya wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres.