Pata taarifa kuu
DRC-MAUAJI-USALAMA

Watu zaidi ya 23 wauawa wilayani Beni

Vyama vya kiraia wilayani Beni, mashariki mwa Jamhuri ay Kidemokrasia ya Congo, vinabaini kwamba mashambulizi ya watu wanaosadikiwa kuwa waasi wa uganda wa ADF yamekithiri wilayani humo.

Askari wa jeshi la DRC (FARDC), katika kijiji cha Eringeti, wilayani Beni, mkoani Kivu Kaskazini (Picha ya zamani).
Askari wa jeshi la DRC (FARDC), katika kijiji cha Eringeti, wilayani Beni, mkoani Kivu Kaskazini (Picha ya zamani). MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Raia wamekua wakilengwa na mashambulizi hayo ya watu wanaobebelea bunduki au mapanga. raia wanashtumu waasi wa Uganda wa ADF, kuhusika na mauaji katika eneo hilo la mashariki mwa DR Congo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Tarehe 24 na 25 Desemba kulitokea mashambulizi yaliyoendeshwa na watu waliokua wakibebelea bunduki mapanga na visu. mashambulizi hayo yaligharimu maisha ya watu 23 na wengine wanane hawajulikani walipo.

"Utaratibu wanaotumia ni ule ule, kwa sababu wanatumia shoka, mapanga kwa kuwaangamiza wakazi wa maeneo ya wilaya ya Beni, anasema Mchungaji Gilbert Kambale, mmoja wa viongozi wa vyama vya kiraia wilayani Beni. Waasi hao wanaendesha vitendo hivyo viovu wakati ambapo askari wa FRAD wanakua hawapo katika maeneo hayo. Waasi hao walionekana pia mchana wa Jumapili katika kijiji cha Tamboko, amesema Mchungaji Gilbert Kambale. Jitihada zinahitajika ili kuonyesha vikosi vya ulinzi na usalama ambapo waasi wanajificha. Ni jeshi kwenda kuwasaka wahalifu hawa. Raia wamekata tamaa, na hana imani na jumuiya ya kimataifa hata serikali ya DR Congo. "

Ongezeko la mashambulizi limesababisha wakazi engi kukimbia na hali hii inamtia wasiwasi Gilbert Kambale. "Inapofika jioni, raia wanaamua kulala karibu na kambi za kijeshi. Watu wamelazimika kuvihama vijiji vyao, na mashamba yao. Raia hao anahitaji misaada ya kibinadamu. Tunajiuliza jinsi gani uchaguzi utafanyika wakati ambapo watu wameyahama makazi yao, baadhi wamekimbilia Ituri, wengine katika maeneo ya Lubero na Butembo. Hayo yote, yanatia wasiwas. Tunaomba jumuiya ya kimataifa na serikali ya DR Congo kurejesha amani, ili watu washiriki uchaguzi katika hali ya utulivu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.