Pata taarifa kuu
CHAD-MAREKANI-USALAMA

Milio ya risasi yasikika kwenye ubalozi wa Marekani nchini Chad

Ubalozi wa Marekani mjini N'Djamena, mji mkuu wa Chad, umeshambuliwa kwa risasi Jumatano hii asubuhi. Hata hivyo hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa. Maafisa wa ubalozi, ambao walikuwa wakiendesha kazi yao, walitakiwa kubaki katika jengo la ubalozi huo.

Geeta Pasi, balozi wa Marekani nchini Chad.
Geeta Pasi, balozi wa Marekani nchini Chad. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mtu anayedaiwa kuhusika na shambulio hilo alikamatwa na kupelekwa kwenye makao makuu ya polisi,kisha kwenye makao makuu ya Idara ya ujasusi kwa kusikilizwa, kwa mujibu wa serikali ya Chad.

Mtu, raia wa Chad, alikuwa amepanda kwenye pikipiki wakati alifyatua risasi akielekeza kwenye ubalozi wa Marekani, mita mia moja kutoka Ikulu ya rais wa Chad.

Katika waraka aliyokutwa nao, mtuhumiwa huyo aikua alijiunga na kundi la Islamic State, chanzo kilio karibu na uchunguzi kimebaini.

Kwa mujibu wa polisi, silaha iliyotumiwa ni bastola iliyotengenezwa nchini Uturuki.

Ubalozi wa Marekani ulikuwa ulizingirwa na vikosi vya usalama baada ya tukio hilo.

Itakumbukwa kwamba mwezi Juni 2015, makao makuu ya polisi na chuo cha polisi katika mji muu wa Chad vilishambuliwa, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya ishirini na zaidi ya 100 kujeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.