Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Angola ya ahirisha kesi ya watuhumiwa 35 waliotaka kuipindua Serikali

media Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos. DR

Serikali ya Angola, Ijumaa ya wiki hii imeahirisha kesi dhidi ya watuhumiwa 37 ambao wanadaiwa kuwa wapiganaji wa zamani wa kundi la upinzani UNITA, ambao wanatuhumiwa kupanga njama za jaribio la mapinduzi mwezi Januari mwaka huu.

Kesi dhidi ya watuhumiwa hao imesogezwa mbele hadi Desemba 2 mwaka huu, kufuatia ombi la upande wa mawakili wa utete, mbele ya jaji wa mahakama kuu ya jijini Luanda, Joao Pedro Fuantoni.

Katika tangazo la kushtukiza, kituo cha taifa cha televisheni kiliripoti kuwa watuhumiwa hao wa kundi la UNITA, wanadaiwa kuwa walipanga njama kuipindua Serikali ya rais Jose Eduardo dos Santos, mwezi Januari.

Wanatuhumiwa kupanga kutekeleza mashambulizi kwenye makazi ya rais jijini Luanda, pamoja na kutaka kushambulio kituo cha taifa cha redio na televisheni.

Kundi la UNITA ambalo lilikuwa kundi kuula waasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu nchini humo kwa takribani miaka 27, hivi sasa ni chama cha upinzani na kimekanusha kuhusika.

Jaji Fuantoni amesema kuwa watuhumiwa hao 35 walikamatwa na vyombo vya usalama na wengine wawili bado wanatafutwa baada ya kutoroka.

Wanakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na uhalifu, jaribio la mauaji ya rais pamoja na kuwa na silaha za kivita kinyume cha sheria.

Rais dos Santos, mwenye umri wa miaka 74, ameliongoza taifa hilo linalosifika kwa utajiri wa mafuta barani Afrika kwa mkono wa chuma kwa kipindi cha miaka 37 sasa.

Nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu mwakani na rais dos Santos anatarajiwa kuwania tena kiti hicho.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana