Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-WAKIMBIZI

Cote d'Ivoire yaanza sensa ya wakimbizi katika ardhi yake

Nchini Cote d'Ivoire, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na serikali ya Cote d'ivoire walizindua Jumanne, Novemba 22 mjini Abidjan, zoezi la usajili wa wakimbizi wanaoishi nchini Cote d'Ivoire, kupitia njia ya shirika la msaada na huduma kwawakimbizi na watu wasiokuwa na uraia (Saara).

Sensa ya wakimbizi wanaoishi nchini Cote d'Ivoire imeanza mjini Abidjan.
Sensa ya wakimbizi wanaoishi nchini Cote d'Ivoire imeanza mjini Abidjan. AFP/Sia Kambou
Matangazo ya kibiashara

Hii ni operesheni ya ukaguzi ili kukusanya maelezo yenye kuaminika kuhusu wakimbizi nchini Cote d'Ivoire. Kwa mujibu wa daktar Lacina Kouakou Kouamé, mratibu wa Shirika la msaada na huduma kwa wakimbizi na watu wasiokuwa na uraia (Saara), zoezi hili litapelekea kuwepo na usimamizi bora wa wakimbizi wanaoishi nchini humo.

"Mahitaji ya wakimbizi ni mengi katika suala la mahitaji ya kijamii. Kuna masuala ya afya, elimu, makazi. Ni kwa yote hayo tunapaswa kuyapa kipaoumbele, kwa mara tu tutakapo pata maelezo kamili. "

UNHCR inaona, kupitia zoezi hili, kutoa ulinzi muhimu ambao wanahitaji wakimbizi. Francis Konan Djaha, afisa katika ngazi ya taifa katika anayehusika na ulinzi katika shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi (UNHCR) anakumbusha kwamba 'UNHCR ni msaada wa kinga.' "Tunalinda watu ambao ni wakimbizi nchini Cote d'Ivoire, amesema. Tangu tu serikali ya Cote d"ivoir ilikubali kuwapokea wakimbizi katika ardhi yake, UNHCR imekua ikitoa msaada wa kiufundi na kifedha, kusaidia wakimbizi. "

Cote d'Ivoire kwa muda mrefu iliwapokea maelfu ya wakimbizi kutokana na migogoro iliyokua ikijiri katika nchi jirani na mahali pengine. Nchi hizi ni hasa Liberia, Sierra Leone, Nigeria, au Libya. Wakimbizi kutoka nchi hizi wanakadiriwa kufikia 2000 waishio katika ardhi ya Cote d'Ivoire katika kusubiri mazingira mazuri kwa ajili ya kurudi katika nchi zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.