Pata taarifa kuu
CONGO-UKIMBIZI

Congo yakataa kutoa hifadhi ya ukimbizi kwa watu zaidi ya 1,500

Serikali ya Congo imekataa kuwapa hifadhi ya wakimbizi watu zaidi ya 1,500, ikibaini kwamba wanaishi nchini humo kinyume cha sheria. Hii ni mara ya kwanza Congo kukataa kanuni ya ukimbizi kwa idadi kubwa ya watu wanaotafuta hifadhi.

Raia kutoka DRC wakiwasili nchini Congo-Brazzaville mwezi Desemba 2011, wakikimbia ghasia za uchaguzi katika nchi yao.
Raia kutoka DRC wakiwasili nchini Congo-Brazzaville mwezi Desemba 2011, wakikimbia ghasia za uchaguzi katika nchi yao. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wengi wa wakimbizi hao ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Miongoni mwao pia kuna raia wa Cote d'Ivoire, na wengine kutoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na Rwanda.

Baadhi wanaishi miaka mingi nchini Congo-Brazzaville.

Mwanasheria wa zamani Kimankutu Asani, kutoka Jamhuro ya Kidemokrasia ya Congo ni miongoni mwa wakimbizi ambao wana mingi wanaishi nchini Congo-Brazzaville.

"Hali yangu ya maisha ni ngumu sana. Na sijui nifanyeje", aamelaumu Bw. Kimankutu.

"Watu hawa wanaotafuta hifadhi wameendelea kuwa na hofu ya kurejea katika nchi zao ambapo hali imeboreka," Tume ya Congo kuhusu Uhakiki kwa kanuni za ukimbizi imebaini katika taarifa yake.

Shirika la haki za binadamu nchini Congo kupitia kiongozi wake Loamba Moke, limeiomba serikali kufanya kilio chini ya uwezo wake ili wakimbizi hao wapewe hifadhi ya ukimbizi.

"Hawana kibali, hawawezi hata kutembea," Amelaumu Bw. Moke.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.