Pata taarifa kuu
TABIA NCHI

WMO: Mwaka 2016 kuvunja rekodi ya mwaka wenye joto zaidi kidunia

Shirika la kimataifa la hali ya hewa duniani, WMO, limesema kuwa mwaka 2016 unatarajiwa kuwa ndio mwaka uliovunja rekodi kuwa na joto, ambapo kwa wastani joto linakaridiwa kuvuka nyuzi joto 1.2 zaidi katika dunia inayojiandaa kuwa ya viwanda. 

Mkurugenzi mtendaji wa jopo la wachambuzi wa mabadiliko ya tabia nchi, Bill Hare, akizungumza akiwa mjini Marrakech.
Mkurugenzi mtendaji wa jopo la wachambuzi wa mabadiliko ya tabia nchi, Bill Hare, akizungumza akiwa mjini Marrakech. REUTERS/Youssef Boudlal
Matangazo ya kibiashara

"Ikiwa hili litathibitishwa, karne ya 21 itahesabika sambamba na ile ya 16 na 17 kwa kuwa miaka iliyokuwa na joto zaidi toka ulipoanza kufanyika utafiti wa kisayansi wa aina hii," imesema taarifa ya WMO, shirika linalotegemewa umoja wa mataifa katika karne ya 19.

"Kila kitu kinaonesha ishara kuwa, mwaka 2016 utakuwa ni mwaka wenye joto zaidi" kwa kuwa na wastani wa joto zaidi ya kile kiwango kilichorekodiwa mwaka 2015," imeongeza taarifa ya shirika hilo, iliyotolewa kando na mkutano wa umoja wa Mataifa wa COP22 unaoendelea mjini Marrakech, Morocco.

Zaidi ya nchi 190 zinakutana mjini Marrakech kujaribu kufikia makubaliano na kuanza kutekeleza mkataba wa makubaliano ya Paris, mkataba uliotiwa saini mwaka uliopita ukilenga kudhibiti hali ya joto kwa angalau nyuzi joto 2.

Wapatanishi wanaoshiriki kwenye mazungumzo ya Marrakech, wanasema itakuwa vigumu sana kwa kila nchi kutekeleza mkataba wa Paris, lakini pia kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi ambayo imeendelea kubadili sura ya dunia, wamesema wataalamu wa mazingira.

Waandamanaji wakijumuika na wanaharakati wa mazingira wakitaka dunia idhibiti ongezeko la joto duniani.
Waandamanaji wakijumuika na wanaharakati wa mazingira wakitaka dunia idhibiti ongezeko la joto duniani.

Hali ya joto kidunia iliongezeka mara dufu mwaka 2015/2016 kutokana na dunia kukumbwa na kipindi cha El Nino, imeainisha ripoti ya WMO.

El Nino ni hali ya kuongezeka kwa joto kwenye mstari wa Ikweta katika bahari ya Pacific, kipindi ambacho kinakadiriwa kuwa hujirudia kila baada ya miaka 5, hali hii ilianza kushuhudiwa katikati ya mwaka huu.

Zaidi ya hali ya joto kidunia, viashiria vingine vya mabadiliko ya tabia nchi pia vilionesha kufikia kiwango cha juu, limeonya shirika hili.

Kiwango cha uharibifu wa tabaka la hewa kwenye uso wa dunia pia kilifikia kiwango cha juu zaidi, kiasi ambacho barafu kwenye bahari ya Artic kupungua kwa kiasi kikubwa na kuanza kuyeyuka, jambao ambalo lilikuwa ni ishara tosha ya athari za kimazingira na tabia nchi.

Mwaka 2016, barafu kwenye bahari ya Artic ilirekodiwa katika kiwango cha chini zaidi, kiasi imefikia kilometa za mraba milioni 4.14 kwa mwezi Septemba, kufuatia kile kipindi cha mwaka 2012.

Ramani inayoonesha mfano wa joto litakavokuwa kidunia.
Ramani inayoonesha mfano wa joto litakavokuwa kidunia. Reuters/路透社

WMO inasema kuwa kilichobaki sasa ni kwa nchi za dunia kuona umuhimu wa kupunguza matumizi ya hewa za ukaa ambazo kwa sehemu kubwa ndizo zimesababisha madhara yanayoshuhudiwa sasa.

Shirika hili limeongeza kuwa, mkutano wa Marrakech ni lazima utoke na maazimio ya namna bora ya kuanza utekelezaji wa mkataba wa Paris, bila kubagua baadhi ya nchi kama ambavyo imekuwa ikishuhudiwa katika utekelezaji wa mikataba mingine ya kimazingira.

Kuongezeka kwa joto duniani, kumesababisha baadhi ya nchi kwenye bara la Asia watu kupoteza maisha huku kwenye ukanda wa Afrika, hali ya ukame ikishika hatamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.