Pata taarifa kuu
DRC-KABILA-UN

DRC: Waziri mkuu Ponyo ajiuzulu, Kamerhe anahusishwa kurithi kiti hicho

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Matata Ponyo, ametangaza kujiuzulu nafasi yake, ili kupisha uteuzi wa waziri mkuu mpya ambaye atatoka kwa vyama vya upinzani vilivyoshiriki mazungumzo ya kitaifa.

Waziri mkuu wa DRC aliyejiuzulu nafasi yake, Augustin Matata Ponyo, hapa ni Kinshasa, 25 Januari  2014.
Waziri mkuu wa DRC aliyejiuzulu nafasi yake, Augustin Matata Ponyo, hapa ni Kinshasa, 25 Januari 2014. AFP/Junior D. Kannah
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza jijini Kinshasa, waziri mkuu Matata Ponyo amesema "nimewasilisha barua yangu ya kujiuzulu kwa rais pamoja na baraza langu lote la mawaziri, ili kutimiza matakwa ya makubaliano ya kitaifa yaliyoafikiwa hivi karibuni," alisema Matata baada ya kukutana na rais Josephu Kabila.

Kujiuzulu kwake ambako kunaenda sambamba na makubaliano ya kumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo, kumefanyika wakati ambapo makubaliano hayo yanapingwa vikali na muungano wa upinzani unaoongozwa na Etienne Tshisekedi wa Mulumba.

Fukuto la joto la kisiasa liliongezeka zaidi mwezi uliopita baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu ambao kwa mujibu wa katiba ulikuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu lakini sasa umeahirishwa hadi mwezi April 2018.

Kiongozi wa upinzani nchini DRC, Vital Kamerhe ambaye ametengwa na muungano wa upinzani
Kiongozi wa upinzani nchini DRC, Vital Kamerhe ambaye ametengwa na muungano wa upinzani DR

Upinzani unamtuhumu rais Kabila, ambaye amekuwa madarakani toka mwaka 2001 kwa kuichezea katiba ya nchi hiyo ili asalie madarakani wakati muhula wake wa pili na wa mwisho utakapotamatika.

Uamuzi wa kuahirisha uchaguzi, ulichukuliwa mwezi Octoba mwaka huu na Serikali, uamuzi ambao ukasababisha kuundwa kwa timu maalumu itakayoshiriki mazungumzo ya kitaifa ili kupata suluhu, makubaliano ambayo hata hivyo yamekashifiwa na baadhi ya viongozi wa upinzani.

Rais Josephu Kabila anatarajiwa kulihutubia taifa Jumanne ya wiki hii, Novemba 15, katika hotuba atakayoitoa bungeni.

Etienne Tshisekedi, kiongozi wa muungano wa upinzani unaopinga makubaliano ya kitaifa, hapa ni Novemba 1, 2016
Etienne Tshisekedi, kiongozi wa muungano wa upinzani unaopinga makubaliano ya kitaifa, hapa ni Novemba 1, 2016 RFI/Sonia Rolley

Ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa Mataifa ulioko nchini DRC, umetoa wito wa mabadilishano ya amani ya utawala nchini humo, kufuatia hofu ya kuzuka vurugu.

Kiongozi wa chama cha UNC, Vitaly Kamerhe ambaye chama chake kilishiriki kwenye mazungumzo hayo ya kitaifa, anatajwa tajwa kuchukua mikoba ya waziri mkuu Matata Ponyo.

Katika mawaziri wakuu wote ambao nchi ya DRC imewapata kwa kipindi cha miaka 56 iliyopita, Matata Ponyo ndiye waziri mkuu pekee ambaye amedumu kwa kipindi kirefu katika wadhifa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.