Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA

Raisi wa Afrika Kusini Jacob Zuma asema haogopi kwenda jela

Raisi Jacob Zuma wa Afrika Kusini ambaye ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu wachunguzi kubainisha uwepo wa ufisadi katika serikali yake,raisi Zuma amewaambia wafuasi wake kuwa haogopi kwenda jela kwa sababu amewahi kufungwa jela kipindi cha ubaguzi wa rangi.

Raisi wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Raisi wa Afrika Kusini Jacob Zuma REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Akihutubia wafuasi wa chama cha ANC huko Dumbe jimboni Kwazulu Natal raisi Zuma amesema amewahi kutumikia miaka mingi jela,hivyo haogopi.

Zuma ambaye alitumikia kifungo cha miaka 10 jela akiwa na muasisi wa taifa hilo Nelson Mandela kipindi cha kupinga ubaguzi wa rangi,amewashutumu wapinzani kutumia mahakama kumtishia.

Jumatano iliyopita Ofisi ya Mwendesha mashtaka wa umma na mkaguzi wa mali ya umma aliwataka majaji kuchunguza ikiwa raisi Zuma,mawaziri na baadhi ya mashirika ya serikali yalikiuka taratibu katika mienendo yao na mfanyabiashara tajiri wa India.

Ndugu za Gupta, Ajay, Atul na Rajesh, ambao ni marafiki wa Zuma na hufanya kazi na mwanae wametuhumiwa kwa kushawishi uteuzi wa mawaziri madai ambayo raisi Zuma ameyapinga.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.