Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

HRW: Serikali ya Gambia isitumie vitisho dhidi ya upinzani na vyombo vya habari

media Rais wa Gambia, Yahya Jammeh akihutubia kwenye umoja wa Mataifa, 27 September 2013. UN Photo/Amanda Voisard

Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu la Human Right Watch, limesema kuwa hakuna uwezekano wowote kwa nchi ya Gambia kufanya uchaguzi uliokuwa huru na haki kutokana na vitisho vinavyotolewa dhidi ya upinzani na vyombo vya habari nchini humo.

Ripoti ya Human Right Watch inatolewa ikiwa ni mwezi mmoja tu umebaki kabla ya nchi ya Gambia kufanya uchaguzi mkuu, uchaguzi ambao utashuhudia Rais wa nchi hiyo, Yahya Jammeh akiendelea kusalia madarakani kwa muhula wa tano.

Shirika hilo linasema kuwa, kutokana na hali inayoendelea kushuhudiwa nchi humo na namna ambavyo Rais Jammeh anatumia vikosi vya nchi yake kuwatisha upinzani na vyombo vya habari, hakuna uwezekano wa nchi hiyo kuwa na uchaguzi uliokuwa huru.

Human Right Watch inasema kuwa, vitisho vinavyoendelea kutolewa dhidi ya upinzani na vyombo vya habari, vinawaweka wanasiasa na vyombo vya habari kwenye hali ya taharuki kwakuwa wanashindwa na wanakosa uhuru wa kuikosoa Serikali ya Rais Jemmeh.

Toka mwezi April mwaka huu, wanaharakati na wanasiasa kutoka vyama vikuu vya upinzani nchini Gambia, wamekuwa wakikamatwa na vyombo vya usalama, kila mara walipokuwa wakijaribu kufanya maandamano ya amani, huku watu wawili kati yao wakiwa wamepoteza maisha kizuizini.

Upinzani umeruhusiwa kufanya maandamano katika majuma mawili ya mwanzo wa mwezi November na ndio siku pekee ambayo vyombo vya habari nchini humo vilifanikiwa kuripoti habari zinazowahusu wapinzani.

Tuhuma za Human Right Watch zinakuja wakati huu ambapo vyama vya upinzania nchini Gambia vimetangaza kuungana na kuchagua Adama Barrow kuuwakilisha na kuchuana na Rais Jammeh kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana