Kiongozi wa Ansar Dine atangaza kusitisha vita
Kiongozi wa waasi wa kundi la Ansar Dine nchini Mali, amekubali kukomesha mashambulizi kaskazini mwa nchi hiyo yaliyosababisha vifo vya raia wa kawaida, wanajeshi wa serikali na wale wa Umoja wa Mataifa.
Imechapishwa:
Kundi la Ansar Dine ambalo limekuwa likishirikiana na kundi la Al Qaeda, limekuwa likitekeleza mashambulizi kaskazini mwa Mali tangu mwaka 2012, kabla ya kuonekana kuelemewa na wanajeshi wa Ufaransa.
Mwandishi wa RFI mjini Bamako nchini Mali Serge Daniel amesema kuwa mwenyekiti wa Baraza la kitaifa la Waisilamu nchini Mali, Mahamoud Dicko, ameliambia shirika la habari la Uingereza la Reuters kuwa, kiongozi wa Ansar Dine, Iyad Ag Ghali, anatarajiwa kuifamisha serikali ya Bamako.