Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Korea Kaskazini yarejea kwenye muungano wa Korea mbili (Seoul)
Afrika

Mapigano makali yazuka mjini Bangui

media Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa karibu na eneo jirani la kata ya PK5 mjini Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. REUTERS/Siegfried Modola

Nchini Jmahuri ya Afrika ya Kati, mapigano makali yalitokea Jumapili jioni Oktoba 30 katika kitongoji cha PK5 mjini Bangui, mji mkuu wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa vyanzo rasmi, makundi matatu ya wanamgambo yalipambana. Angalau watu kumi, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa kundi moja waliuawa, na wengine wengi kujeruhiwa.
 

Jumapili, Oktoba 30 kwenye saa 11:30 (saa za nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati) na kwa muda wa zaidi ya saa moja, milio ya risasi ilisikia katika kitongoji cha PK5, kitongoji wanakoishi Waislamu wengi. Chanzo cha Umoja wa Mataifa kimethibitisha kuwa zilisikika bunduki aina ya RPG.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, makabiliano hayo yalikua kati ya makundi ya wanamgambo ya Mohammed Ali Fadul na mawili yanayoongozwa na Kapi Issa, almaarufu 50-50, na Abdul Danda, anayetuhumiwa kutekeleza mauaji ya kiongozi wa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati (Faca), Marcel Mombeka, mapema mwezi huu. Mauaji ambayo yalisababisha ulipizaji kisasi na kuzuka kwa ghasia, ambapo watu kadhaa waliuawa.

Haijajulikana bado sababu sahihi ya makabiliano haya, lakini kwa mujibu wa chanzo cha Umoja wa Mataifa, huenda ni kutokana na "kutoelewana" kati ya makundi hayo tofauti. Lakini haijajulikana nani alianza kushambulia mwengine na kwa nini.

Hata hivyo, kwa mujibu wa wakazi kadhaa wa kitongoji hiki waliohojiwa kwa simu na RFI, hali ya utulivu inaonekana kurejea tangu baada ya makabiliano hayo kumalizika. Lakini wakazi wa kitongoji cha PK5 wamesalia nyumbani kwa uoga na hofu ya kuzuka kwa mapigano mapya. Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kimetuma askari wake katika kitongoji hiki.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana