Pata taarifa kuu
CAR_MINUSCA-USALAMA

Watu wanne wauawa mjini Bangui

Raia wanne wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea katika mji wa Bangui ambapo mashirika ya kiraia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yalikua yalitoa wito wa kusalia nyumbani kwa ajili ya kuomba kuondoka kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo.

Kikosi cha Umooja wa Mataifa kikipiga doria katika mji wa Bangui Januari 2, 2016.
Kikosi cha Umooja wa Mataifa kikipiga doria katika mji wa Bangui Januari 2, 2016. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kinashtumiwa kushindwa kuyazima au kuyadhibiti makundi ya watu wenye silaha.

"Askari wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) waliingilia kati mapema Jumatatu hii katika mji wa Bangui ili kuondoa vizuizi vilivyokua vimewekwa barabarani na waandamanaji wanaowapinga," Minusca imebaini katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu hii jioni.

"Minusca inalaani kabisa matukio ambayo yaliathiri baadhi ya maeneo ya mji mkuu na inasikitishwa kuona hali hiyo imesababisha vifo vya raia wanne na kuwajeruhi wengine 14, ikiwa ni pamoja na askari watano wa kikosi cha Umoja wa Mataifa, " taarifa hiyo imeongeza. Vurugu hizi "ni jaribio mpya la maadui wa amani kwa lengo la kuvuruga kurejea kwa hali ya kawaida ya kikatiba."

Minusca "pia inafutilia mbali kampeni ya kupakwa matope dhidi askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani na itaendelea na kazi yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Minusca pia inakumbusha kwamba vurugu zozote zile dhidi ya askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani zitapelekea wahusika kufunguliwa mashtaka katika mahakama za kimataifa," taarifa hiyo imehitimisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.