Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-USALAMA

Silaha zinazoingizwa nchini Sudan Kusini zaendelea kuchochea vita

Wakati ambapo Baraza la Usalama likiendelea kujadili uwezekano wa vikwazo vya silaha dhidi ya Sudan Kusini, ripoti ya wataalamu inaonyesha kwamba silaha zinazoingia nchini Sudani Kusini zikitokea Ulaya ya Mashariki na Israel zimekua zikipitia nchini Uganda na Senegal. Silaha hizi zimekua zikipewa serikali pamoja na upinzani.

Askari wa Riek Machar wakisherehekea katika mji wa Lalo, kusitishwa kwa mapigano, Oktoba 16 2016.
Askari wa Riek Machar wakisherehekea katika mji wa Lalo, kusitishwa kwa mapigano, Oktoba 16 2016. REUTERS/Jok Solomon
Matangazo ya kibiashara

Moja ya viwanda vya silaha vinavyooingiza silaha nchini Sudan Kusini kimetambuliwa rasmi.

Mwezi Agosti 2016, mapigano makali na vikosi vya serikali yalisababisha askari wa Makamu wa zamani wa rais Riek Machar kutoroka nchi hiyo na kukimbilia nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wakati huo tume ya Umoja wa Mataifa nchini DR Congo iliwapokonya silaha askari wa Bw Machar wakati ambapo silaha hizo waliokua nazo zilikua na namba moja ya usajili inayojifanana. Kwa mjibu wa wataalamu wa Umoja wa Mataifa, silaha hizo zilitoka katika ghala la silaha zilizouzwa na Israel mwaka 2007 kwa Wizara ya Ulinzi nchini Uganda. Silaha hizi zilisafirishwa nchini Sudan Kusini kwa niaba jeshi la serikali na kwa bahati mbaya zilikamatwa na askari wa Riek Machar.

Machar kwa upande mwengine alijaribu kupata silaha kupitia angalau njia nyingine. Uhispania ilitaarifu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Makamu wa zamani wa rais alinunua silaha za kivita kwenye soko lisilokua halali katika Ulaya ya Mashariki kupitia raia mmoja wa Senegal.

Hatimaye, ripoti inaeleza kuwa mwaka 2014 bunduki 4 000 za kivita zilinunuliwa kutoka kiwanda kimoja nchini Bulgaria ili kusafirishwa nchini Uganda. Lakini silaha hizi, ziliingizwa nchini Sudan Kusini. Ripoti hii itapelekea kuanzishwa majadiliano mapya juu ya vikwazo vya silaha nchini Sudan kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.