Pata taarifa kuu
ICC-DRC-BEMBA

ICC: Jean-Pierre Bemba akutwa na hatia ya kuhonga mashahidi

Mahakama ya Kimataifa ilitoa Jumatano, Oktoba 19 uamuzi wake juu ya raia wa DR Congo Jean-Pierre Bemba. Mahakama hii imebaini kwamba Bw Bemba na wanasheria wake Aimé Kilolo na Jean-Jacques Mangenda, walikutwa na hatia ya kuwahonga mashahidi katika kesi ya aliyekuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Jean-Pierre Bemba,mbele ya Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, mjini Hague.
Jean-Pierre Bemba,mbele ya Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, mjini Hague. AFP/MICHAEL KOOREN
Matangazo ya kibiashara

Jumatano hii Bw Bemba amehukumiwa kwa kuwashaiwshi mashahidi baada ya kupewa khongo na kubadilisha ushahidi katika kesi inayomkabili katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa KIvita.

Washirika wake wanne wa karibu pia wameutwa na hatia.

Itafahaamika kwamba Mwezi Machi mwaka huu Bemba alipatikana na hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadmu aliotekeleza nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya mwaka 2002 na 2003. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) ilimuhukumu kifungo cha miaka 18 jela.
Hata hivyo Jean-Pierre Bemba alipinga uamuzi huo na aliamua kukata rufaa.

Alituhumiwa kwa kushindwa kuvikataza vikosi vyake vya waasi ambavyo vilishutmiwa kuwaua na na kuwabaka wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.