Pata taarifa kuu
DRC-EU-SIASA

Uchaguzi nchini DRC: EU yatoa shinikizo kwa serikali ya Kinshasa

Umoja wa Ulaya umetoa shinikizo kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi 28 za Umoja huo wameiomba serikali ya Kinshasa kuandaa haraka iwezekanavyo uchaguzi katika mwaka 2017.

Bendera za EU nje ya makao makuu ya Tume ya Ulaya.
Bendera za EU nje ya makao makuu ya Tume ya Ulaya. REUTERS/Thierry Roge
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri hawa wanaokutana mjini Luxembourg, wametoa kauli yenye maneno makali na pia wametishia kuwachukulia vikwazo baadhi ya watu ambao watakua ni pingamizi kwa nchi hiyo kuondoka katika mgogoro unaoendelea.

Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi 28 za Umoja wa Ulaya wamekubaliana kutoa kauli ya pamoja kwa kumshinikisha Rais Joseph Kabila kufanya kile kilio chini ya uwezo wake ili mgogoro unaoendelea nchini DR Congo umalizike haraka iwezekanavyo. Kwa upande wa nchi za Umoja wa Ulaya, vitendo vya vuruguvilivyosababisha vifo vya watu wengi tarehe 19 na 20 Septemba katika mji wa Kinshasa nimechangia kuongezeka kwa mgogoro uliyotokana na kutoitishwa kwa uchaguzi wa urais ndani ya muda uliowekwa na Katiba ya nchi hiyo, ambapo Umoja wa Ulaya unanyooshea kidolea cha lawama serikali ya DR Congo kuhusika na hali hii.

Katiba inapaswa kuhemishwa na pande zote husika, hasa kwa suala la kikomo cha idadi ya mihula ya rais kukaa madarakani. Vile vile, mazungumzo ya kisiasa yatapelekea kufanyika kwa uchaguzi wa urais na wa wabunge kabla ya mwisho wa mwaka 2017. Wakati huo huo, makubaliano chini ya upatanishi wa Umoja wa Afrika yanapaswa kuandaa kipindi cha mpito.

Makundi yote ya kisiasa yanapaswa kushiriki, sawa na vyama vya kiraia, ikiwa ni pamoja na Baraza Kuu la Maaskofu nchini DR Congo. Hatimaye, Umoja wa Ulaya imeitaka serikali kukomesha haraka iwezekanavyo mauaji na mateso dhidi ya wanasiasa wa ipinzani na waandishi wa habari. Orodha ya watu waliohusika katika vitendo hivyo itawekwa wazi kulingana na uzito wa vitendo hivyo na orodha hiyo itawasilishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.