Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MISRI-USALAMA

Serikali ya Ethiopia yaituhumu Misri

Ethiopia imetuhumiwa 'maadui zake wa nje' kuwa chanzo cha vurugu zinanzoendelea kulikumba taifa hilo na kupelekea Jumapili Oktoba 9 serikali kutangaza hali ya hatari kwa miezi sita. Addis Ababa inailenga hasa Misri. Tuhuma hizi zinaonekana kuwa ni nzito kwa serikali ya Misri.

Polisi katika mji wa Bishoftu, kusini mwa mji wa Addis Ababa, Oktoba 2, 2016
Polisi katika mji wa Bishoftu, kusini mwa mji wa Addis Ababa, Oktoba 2, 2016 Zacharias ABUBEKER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mahusiano yalikuwa tayari tete kati ya Ethiopia na Misri kwa sababu ya bwawa kubwa la Renaissance nchini Ethiopia limekua likijengwa karibu na mto Nile. Leo, serikali ya Addis Ababa inaituhumu Misri kuhusika moja kwa moja katika machafuko yaliyozuka katika jimbo la Oromo, na kusaidia waasi wanaotaka kujitenga kwa jimbo hilo wa OLF (Oromo Liberation Front).

"Tuna ushahidi wa wazi kwamba kulikua na mazoezi na mafunzo yaliyofadhiliwa na Misri. Hatusemi kwamba Misri inahusika moja kwa moja, lakini tunajua kwa uhakika kwamba kundi la kigaidi la OLF lilipata kila aina ya msaada kutoka Misri. Kabla viongozi wa kundi hili walikuwa katika mji wa Asmara, kwa sasa wako katika mji wa Cairo, "amesema msemaji wa serikali, Getachew Reda. "Makundi ya kigaidi yalipewa kila aina ya maelekezo ili kuyumbisha usalama nchini Ethiopia na kutuzuia kumaliza ujenzi wa bwawa la Renaissance," amesema Bw Reda.

Kama hali ya hatari imetangazwa, hatua halisi za kuchukuliwa hata hivyo bado zinajadiliwa. "Hali ya hatari inalenga kujipanga vizuri kwa vikosi vya usalama. Kwa iyo, ndiyo, ina maana kutumwa kwa askari. Hiyo ina maana kuwa hatua mpya zinahitajika ili kutatua mgogoro huu. Kwa mfano, serikali inaweza kufikiria kuwa ni muhimu, katika baadhi ya miji ya kuchukuliwa hatua ya kutotoka nje usiku. Ni aina hii ya hatua ambazo zinatazamiwa kutekelezwa, " Msemaji wa serikali, Getachew Reda, amesema Jumatatu wiki hii.

Hali ya hatari inapaswa kupitishwa na Bunge kwa wingi wa theluthi mbili ya kura katika wiki mbili zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.