Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

ICGLR, AU na UN kukutana kwa minajili ya kutafutia ufumbuzi mgogoro wa DR Congo

Mkutano wa kimataifa wa kutafutia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utafanyika tarehe 26 Oktoba katika mji mkuu wa Angola, Luanda.

Kwa upande wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Georges Chikoti, uchaguzi nchini DRC hautawezekana kwa muda uliyopangwa.
Kwa upande wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Georges Chikoti, uchaguzi nchini DRC hautawezekana kwa muda uliyopangwa. Photo: Chatham House, source: Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu uliyoandaliwa kwa pamoja na jumuiya ya nchi za Ukanda wa maziwa makuu (ICGLR), Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na SADEC, ulikuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu, lakini mapigano ya mwezi Septemba 19, sawa na kuonekana ugumu kwa wanasiasa wa DR Congo kufikia makubaliano juu ya uchaguzi, una maana kubwa kwa mkutano huu wa kilele wa wakuu wa nchi.

Wataalam wa Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Ukanda wa maziwa makuu (ICGLR) watakutana wiki ijayo. Hali ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo bado ni tete. Hii ni moja ya ahadi zilizotolewa na jumuiya ya kimataifa na nchi 14 za Ukanda wa maziwa makuu wakati wa kutiwa saini makubaliano ya mjini Addis Ababa mwezi Februari 2013. Mkutano wa mjini Luanda huenda utakua ni mafaanikio kwa mgogoro unaoikabili wakati huu nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Lakini vifo vya watu kadhaa waliouawa katika maandamano ya Septemba 19, sawa na mazungumzo magumu ya kisiasa mjini Kinshasa, yanaupa taswira mkutano huu wa Wakuu wa Nchi kushughulikia hara mgogoro nchini humo, kama alivyoeleza Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Georges Chikoti. "Hakika kuwa uchaguzi hautawezekana kwa muda uliyopangwa, yaani mwishoni mwa mwaka huu, lakini itachukua kipindi fulani cha taasisi za mpito ili kuhitimisha masuala ya kiufundi na kifedha vinavyokosekana kwa ajili ya uchaguzi. "

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika pamoja na Wakuu wa nchi za ukanda wa Maziwa Makuu wanaweza kutoa msaada wa kiufundi na kifedha ili kuandaa kwa haraka uchaguzi wa rais na wa wabunge.

Hata hivyo, baadhi ya mapendekezo yaliyofikiwa katika mikataba ya mjini Addis Ababa yanakataza kuingilia katika masuala ya ndani ya nchi jirani.

Hali nchini Burundi, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati pia itajadiliwa katika mkutano huu wa kilele mjini Luanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.