Pata taarifa kuu
FATOU BENSOUDA-ICC-AFRIKA

Bensouda: Itakuwa aibu kwa Afrika kujitoa kwenye mahakama ya ICC

Mwendesha mashataka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, amesema kuwa, itakuwa siku ya huzuni kubwa ikiwa nchi za Afrika zitaamua kujitoa kwenye mkataba Roma unaotambua mahakama hiyo, ameliambia shirika la habari la uma la Afrika Kusini, SABC.

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, Fatou Bensouda.
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, Fatou Bensouda. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya mwendesha mashtaka, Fatou Bensouda, inakuja wakati huu ambapo baadhi ya nchi za Afrika zinazishawishi nchi nyingine kujitoa kwenye mahakama hiyo kwa kile wanachodai kuwa mahakama hiyo inawalenga viongozi wa Afrika peke yake.

Akiwa amepewa jukumu la kuhakikisha haki inapatikana kwa waathirika wa makosa ya kivita, Bensouda hata hivyo amejikuta akikosolewa pakubwa na nchi za Afrika akidaiwa kuwalenga kwa makusudi, tuhuma ambazo Bensouda mwenyewe anasema zimemuhuzunisha.

Fatou Bensouda ametoa wito kwa wakuu wa nchi za Afrika kuachana na mpango wao wa kujiondoa kwenye mahakama ya ICC, akisema kufanya hivyo kutawanyima wananchi wengi wa Afrika haki na wahalifu kuendelea kulindwa.

Bensouda ameongeza kuwa, licha ya ukosolewaji ofisi yake inaendelea na kesi kadhaa zilizoko mbele yake na kwamba tayari pia wameanzisha uchunguzi wa awali katika baadhi ya nchi ambako uhalifu dhidi ya binadamu umetekelezwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.