Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI

DRC; Hofu ya kutokea vurugu yatanda baada ya pendekezo la CENI

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, CENI, mwishoni mwa juma, imesema inapanga kuomba kusogezwa mbele kwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge, uliokuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, sasa ufanyike mwenzi November mwaka 2018.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC, Corneile Naanga ambaye amependekeza uchaguzi mkuu usogezwe mbele
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC, Corneile Naanga ambaye amependekeza uchaguzi mkuu usogezwe mbele Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la tume ya uchaguzi nchini DRC, limekuja wakati huu upinzani nchini humo ukihofia kuwa huenda rais Josephu Kabila asiondoke wakati muda wake utakapofikia kikomo mwezi December.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, Corneile Naanga, amesema kuwa wameomba uchaguzi huo usogezwe mbele ili kutoa nafasi ya kufanyika kwa maandalizi mazuri zaidi yatakayopelekea kuwa na uchaguzi ulio huru na haki.

Hata hivyo upinzani tayari umepinga pendekezo hili la tume ya uchaguzi, ambapo kwa majuma kadhaa muungano wa vyama vya siasa nchini humo unaoongozwa na mwanasiasa mkongwe Ettien Tshisekedi umekuwa ukishinikiza uchaguzi kufanyika mwaka huu na rais Kabila kuondoka madarakani kwa mujibu wa katib.

Tangazo hili linatolewa pia, wakati huu mazungumzo ya kitaifa kusaka suluhu ya kisiasa nchini humo yakiendelea kusuasua, huku ikiwa haijulikani ikiwa kutapatikana suluhu, na hasa baada ya tangazo hili la CENI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.