Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Watu kadhaa wafariki katika makabiliano Ethiopia

media Waandamanaji wakidai mwisho wa ukandamizaji dhidi ya watu kutoka jamii ya Oromo, mjini Addis Ababa, Agosti 6, 2016. REUTERS/Tiksa Negeri

Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yamesababisha watu wengi kufariki dunia nchini Ethiopia, wakati wa tamasha la jadi la Oromo Ireecha. Tukio hilo limetokea Jumapili asubuhi katika mji wa Bishoftu, kusini mwa mji wa Addis Ababa, lakini taarifa ya watu waliopoteza maisha bado haijathibitishwa na serikali.

Ni vigumu kusema kwa sasa ni watu wangapi wamepoteza maisha Jumapili hii asubuhi katika mji wa Bishoftu mkoani Oromo, jina la kabila la kwanza kwa watu wengi nchini Ethiopia. Makabiliano yalilipuka wakati wa sikukuu ya kidini inayoashiria mwisho wa msimu wa mvua.

Umati wa watu waliokuepo katika sherehe hizo walipinga uwepo wa viongozi kutoka jamii ya Oromo wanaoshirikiana na serikali, ambao wanawachukulia kama wasaliti. Waandamanaji walijaribu kuvamia jukwaa waliokuemo viongozi hao, lakini polisi walijibu kwa mabomu ya machozi.

Ilifuatiwa hali ya wasiwasi na hofu na kusababisha watu kukanyagana ambapo wakati huo watu kadhaa walipoteza maisha. Mpiga picha wa shirika la habari la AFP anasema aliona miili angalau ishirini ya watu waliofariki.

Upinzani nchini Ethiopia kwa upande wake, unadai kuwa watu zaidi ya 100 walifariki katika mkanyagano huo. Tamasha lilivunjwa na tukio hili linakumbusha hali ya mivutano inayoshuhudiwa katika mkoa wa Oromo wakati ambapo maandamano dhidi ya serikali ambayo yalianza karibu mwaka mmoja uliyopita yameendelea kushika kasi.

Kwenye mitandao ya kijamii, wanaharakati kutoka jamii ya Oromo wametoa wito wa hasira wa siku tano, huku idadi kubwa ya polisi ikionekana Jumapili hii mchana katika mkoa wa Oromo na karibu ya mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana