Pata taarifa kuu
LIBYA-UFARANSA

Ufaransa kuwa mwenyeji wa mkutano kuhusu mzozo wa Libya

Serikali ya Ufaransa imetangaza kwamba itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa kuhusu mzozo wa Libya utaofanyika juma lijalo ambapo mataifa kadhaa za ukanda wa Afrika kaskani ikiwemo Misri na nchi za Ghuba zitashiriki katika mkutano huo muhimu.

Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj, Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani John Kerry na Waziri wa mambo ya Nje wa Italia, wakati wa mkutano kuhusu Libya mjini New York, Septemba 22, 2016.
Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj, Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani John Kerry na Waziri wa mambo ya Nje wa Italia, wakati wa mkutano kuhusu Libya mjini New York, Septemba 22, 2016. REUTERS/Jason DeCrow
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Ufaransa Stéphane Le Foll amesema Waziri wa Mambo ya Nje Jean Marc Ayrault amewaambia mawaziri kutoka Misri, Qatar, Saudia Arabia, Uturuki kwamba ni muhimu kukutana ili kujadili kuhusu hatma ya Libya wakati huu wa mchakato wa muungano wa taifa hilo.

Waziri mkuu mpya wa Libya Fayez al Sarraj ambaye alikutana na rais wa ufaransa jijini Paris hivi majuzi amesema kiongozi wa kijeshi ambae anamiliki bandari muhimu za mafuta kaskazini mwa Libya atawakilishwa katika serikali nyingine mpya inayotarajiwa kuundwa hivi karibuni na kwamba hakuna njia nyingine mbali na mazungumzo pamoja na maridhiano.

Hayo yanajiri wakati huu kukiwa na changamoto za kukabiliana na wapiganaji wa kundi la Daesh nchini libya, ambapo rais wa Ufaransa François Hollande amepongeza vikosi vya wapiganaji wa Libya kufaulu kuwafurusha wapiganaji wa kundi linalojiita Islamic State katika mji wa Syrte.

Serikali ya sasa ambayo inaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa imeshindwa kurejesha uwiano na maridhiano katika taifa hilo lililogawanyika tangu kuuawa kwa rais wa zamani wa Libya hayati Kanali Muamar Gadaffi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.