Pata taarifa kuu
UN-DRC

Umoja wa Mataifa walaani vurugu za mjini Kinshasa

Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein, amesema viongozi wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo wana haja ya kubadili kile alichokiita "msimamo wenye mgogoros" ili kujiepusha na mgogoro mkubwa.

Mwanamfalme Zeid amelaani matumizi ya nguvu, na uchomaji wa makao makuu ya vyama kadhaa vya siasa.
Mwanamfalme Zeid amelaani matumizi ya nguvu, na uchomaji wa makao makuu ya vyama kadhaa vya siasa. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Mwanamfale Zeid amelaani matumizi ya nguvu, na uchomaji wa makao makuu ya vyama kadhaa vya siasa.

Kwa uchache watu hamsini, wengi wao wakiwa wafuasi wa upinzani, wameuawa katika mapigano katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, mwanzoni mwa wiki.

Umoja wa Mataifa unasema idadi hiyo ya vifo inaweza kuwa zaidi ya hiyo.

Siku tatu baada ya ghasia hizo, Rais Kabila aliahidi kutoa "msaada kwa kutumia hatua ya kisheria" dhidi ya watu waliohusika na vurugu hizo.

Rais wa DR Congo ambaye muhula wale unamalizika Desemba 19 alitoa rambirambi zake kwa familia za watu waliojeruhiwa na wale waliouawa wakati wa maandamano yaliyoandaliwa na kuitishwa na upinzani, Jumatatu, Septemba 19 katika mji wa Kinshasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.