Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Ukame, vita na uhaba wa chakula nchini Somalia, watishia baa la njaa

media Baadhi ya familiya ambazo bado zinaishik kwenye makambi mjini Mogadishu, Somalia. REUTERS/Feisal Omar

Raia milioni 5 wa Somalia au zaidi watu wawili katik ya watano kwenye taifa hilo, hawana chakula cha kutosha kula na wanaishi kwenye hali mbaya, imesema taarifa mpya ya umoja wa Mataifa, ikitoa wito wa kuchangishwa kwa fedha zaidi kupata chakula cha msaada.

Takwimu mpya zimeonesha kuwa, kumekuwa na ongezeko la watuj laki 3 zaidi ambao hawana chakula toka mwezi February mwaka huu, imesema taarifa hiyo ya shirika la misaada la umoja wa Mataifa, OCHA.

“Washirika wa misaada ya kibinadamu wako tayari kusaidia familia ambazo zinakabiliana na changamoto ya uhaba wa chakula kwa angalau kupitisha siku moja,” amesema Peter de Clercq, mratibu wa misaada ya kibinadamu kwa nchi ya Somalia.

Ameongeza kuwa mpango wa awali wa kutoa misaada ya kibinadamu ulikuwa ni kuwafikia watu hao kwa asilimia 32 ya fedha ambazo zilipatikana na kwamba fedha za ziada zinahitajika kukabiliana na janga la utapia mlo na upatikanaji wa uhakika wa chakula.

Utafiti uliofanywa na shirika la chakula la umoja wa Mataifa, FAO, limesema kuwa watu zaidi ya milioni 1 na laki 1 hawana uwezo wa kupata mlo wa siku, wakati watu wengine zaidi ya milioni 3 na laki 9 nchini Somalia wanahitaji msaada.

Miongoni mwa watu wanaokabiliwa na njaa, wamo watoto laki 3 ambao wana umri wa chini ya miaka 5 na sasa wanakabiliwa na maradhi ya utapia mlo, wakiwemo watoto zaidi ya elfu 50 ambao wana hali mbaya.

Msimu wa mavuno nchini Somalia umekumbwa na hali mbaya ya ukame ulioikumba nchi hiyo na hasa majira ya El Nino ambayo hutokea kila baada ya miaka mitano hadi saba.

Watu wanaokabiliwa na janga la njaa wanafikia watu milioni 1 na laki 1, ambao hawa walikimbia makazi yao, wengi wakikimbia kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano kwenye baadhi ya maeneo.

Shirika la OCHA limesema kuwa, wengi wa waathirika wanaishi kwenye hali mbaya na kwenye maeneo ambayo yameharibika kutokana na vita.

Mwaka 2012, ukame mkali ulishuhudiwa nchini humo kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambapo watu zaidi ya laki 2 na elfu 50 walikufa kutokana na njaa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana