Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 13/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Hali ya utulivu yarejea nchini DRC, wanasiasa, raia watakiwa kuwa watulivu

media Gari la Polisi nchini DRC likiwa kwenye doria jijini Kinshasa REUTERS/Stringer

Hali ya utulivu imerejea kwenye mijik mingi nchinik Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya nchi hiyo kushuhudia vurugu kubwa zilizotokana na maandamano ya muungano wa vyama vya upinzanik nchini DRC, ambao wanashinikiza kuondoka madarakani kwa Rais Josephu Kabila.

Kwa siku mbili mfululizo nchini ya DRC ilishuhudia maandamano karibu nchik nzima, huku kwenye baadhi ya miji, maandamano yaliyoanza kwa amani, kugeuka na kuwa ya vurugu na hata kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.

Maandamano haya yaliyoanza siku ya Jumatatu, yalishuhudiwa yakiendelea hadi Jumanne ya September 20 jijini Kinshasa, ambako ofisi za chama kikuu cha upinzani cha UDPS pamoja na vyama vingine vidogo, zilichomwa moto.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch, limelaani vurugu zilizojitokeza juma hili, na kukosoa namna ambavyo vyombo vya usalama vilikabiliana na waandamanaji jijini Kinshasa.

Human right watch inasema kuwa shirika lao limerekodi vifo vya watu zaidi ya 37 ambao waliuawa na Polisi wakati wa maandamano hayo, na kuongeza kuwa mamia ya watu wengine wamejeruhiwa.

Baadhi ya waandamanaji nchini DRC, wakishiriki maandamano ya juma hili ambayo baadae yaligeuka vurugu. REUTERS/Kenny Katombe

Vurugu za nchini DRC zilikuwa pia ajenda kwenye hotuba za viongozi kadhaa wa dunia akiwemo Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ambaye ameitaka Serikali ya nchi hiyo kuheshimu katiba ya nchi pamoja na upinzani kujiepusha na kuhamasisha vurugu ambazo zinaweza kuitumbukiza nchi hiyo kwenye machafuko.

Rais Hollande alisema kuwa kinachoendelea kushuhudiwa nchini DRC hakikubaliki, na kwamba ni lazima kwanza nchi yenyewe pamoja na wadau wa mzozo wa nchik hiyo, kukubaliana njia bora ya kumaliza tofauti zao kuliko kukimbilia vurugu.

Umoja wa Mataifa pia umetoa wito kwa Serikali na wadau wasiasa nchini humo, kujiepusha na vurugu, na kutaka kuheshimiwa kwa katiba ya nchi na taifa hilo kuandaa uchaguzi kwa wakati.

Vurugu hizi zinajiri wakati huu ambapo tume ya taifa ya uchaguzi CENI, haijatangaza tarehe rasmi ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, wala Rais Kabila mwenyewe kueleza uma wa DRC ni lini ataondoka madarakani kwa mujibu wa katiba.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana