Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Uhaba wa dawa muhimu wasababisha hospitali kuu ya Harare kuahirisha operesheni

Moja yha hospitali kubwa nchini Zimbabwe imetangaza kusitisha kwa muda kufanya operesheni kwa wagonjwa, baada ya kuishiwa na dawa za maumivu, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Daktari nchini Zimbabwe akivalia vazi la kuingia kufanya upasuaji.
Daktari nchini Zimbabwe akivalia vazi la kuingia kufanya upasuaji. Zimnews.com
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imeendelea kudhihirisha hali mbaya ya kifedha na kiuchumi inayoikabili nchi hiyo, huku shinikizo dhidi ya Serikali likiendelea.

Serikali ya Rais Mugabe inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa fedha, hali ambayo imesababisha kufanyika kwa maandamano makubwa hadi kumlazimisha gavana wa benki kuu ya Zimbabwe kutangaza kuchapisha fedha mpya zitakazoanza kutumika kuanzia mwezi ujao.

Hospitali kuu ya Harare, ambayo ni hospitali ya pili kwa ukubwa nchini humo, imesema sasa itajikita zaidi katika kushughulikia haja za dhalura, chumba cha wagonjwa mahututi na wanawake.

“Kutokana na uhaba wa dawa za pethidine, injectable morphine, adrenaline na antibiotics, imeamuliwa kuwa, tutaahirisha kwa muda baadhi ya operesheni” limeripoti gazeti moja binafsi la NewsDay.

Mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo amenukuliwa na gazeti la Serikali akisema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakitegemea kuendesha shughuli za hospitali hiyo kwa kutegemea fedha zinazolipwa na wagonjwa kwakuwa hawapokei tena ruzuku kutoka Serikalini.

Hivi karibuni Serikali ilitangaza kuwa asilimia 97 ya mapato na matumizi yake hutumia kulipa mishahara pekee.

Nchi ya Zimbabwe ilianza kutumia dola ya Marekani mwaka 2009 baada ya nchi hiyo kushuhudia mfumuko mkubwa wa bei uliofikia asilimia bilioni 500.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.