Pata taarifa kuu
DRC-BOSCO NTAGANDA

Bosco Ntaganda: niko tayari kufa

Septemba 7, 2016 Bosco Ntaganda alianza mgomo wa njaa kupinga dhidi ya uamuzi wa majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Bw Ntaganda anashtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita aliofanya katika eneo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mwaka 2002 na 2003.

Bosco Ntaganda, Februari mwaka 2015, Hague, Uholanzi.
Bosco Ntaganda, Februari mwaka 2015, Hague, Uholanzi. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa waasi wa zamani wa DR Congo amekua akikataa kwenda mahakamani kusikilizwa. Kesi ya Bw Ntaganda ilianza mwaka mmoja uliopita mjini Hague.

"Mimi ni mwanamapinduzi" na "niko tayari kufa," amesema Bosco Ntaganda akiwa katika chumba anakozuiliwa mjini Hague.

Majaji watatu wa Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ya ICC waliongeza muda wa vikwazo viliyochukuliwa dhidi ya mshitakiwa, wakati ambapo alikuwa alishtumiwa kuwarubuni mashahidi wa mwendesha mashtaka, kupitia mfungwa mmoja, aliyewasiliana naye kwa simu kutoka chumba chake anakozuiliwa.

Mawasiliano yake na watu wa nje yanafuatiliwa kwa kina. Anawasiliana na mkewe pamoja na mama yake kwa masaa mawili kwa wiki. Bosco Ntaganda analalamika kwa upande mwengine kwamba haruhusiwi kuwaona watoto zake saba tangu kukimbilia katika ubalozi wa Marekani nchini Rwanda, na kisha kuhamishiwa mjini Hague mwezi Machi 2013. Karani anatafuta hati za kusafiria na visa ili kuruhusu ziara hiyo haraka iwezekanavyo, lakini kiongozi huyo wa zamani wa kivita anadai kuwa "amepoteza matumaini".

Kwa upande wake, upande wa mashtaka umeshutumu kuwa ni "uongo" wa mtuhumiwa, ambaye anataka "kuiteka" Mahakama kwa kuwatia uoga majaji. Upande wa mashtaka, ambao tayari umewafikisha kizimbani mashahidi thelathini na unatarajiwa kuendelea kuwasilisha ushahidi wake katika mwaka 2017.

Kiongozi wa zamani wa waasi wa DR Congo Bosco Ntaganda.
Kiongozi wa zamani wa waasi wa DR Congo Bosco Ntaganda. Reuters

Itakumbukwa kwamba Bosco Ntaganda anashitaka kwa mauaji, ubakaji, uporaji na kuajiri watoto walio na umri uliyo chini ya miaka 15 katika jeshi lake la FPLC, moja ya kundi la wanamgambo waliokua wakiendesha vitendo viovu katika eneo la Ituri mwaka 2002 na 2003. Tuhuma ambazo mtuhumiwa, anayejulikana kwa jina la utani la "Terminator", amekanusha.

Majaji kwa sasa wataamua kama wataendelea au la na kesi iwapo mtuhumiwa ataendelea kukosekana mahakamani.

Bosco Ntaganda, wakati wa sherehe ya kuingiza waasi katika vikosi vya jeshi la DR Congo, mwezi Januari 2009 Kivu Kaskazini.
Bosco Ntaganda, wakati wa sherehe ya kuingiza waasi katika vikosi vya jeshi la DR Congo, mwezi Januari 2009 Kivu Kaskazini. AFP PHOTO/Walter ASTRADA

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.