Pata taarifa kuu
GABON-AU

Ujumbe wa AU nchini Gabon waahirishwa

Umoja wa Afrika umeahirisha kutuma ujumbe wake utakaohusika na kuchangia kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Gabon. Umoja wa Afrika haujaleza tarehe nyingine ambapo ujumbe huo utatumwa, Waziri wa mambo ya Nje wa Gabon, Emmanuel Isozet Ngondet, ametangaza Alhamisi hii Septemba 8.

Mfuasi wa kiongozi mkuu wa upinzani Jean Ping akishikilia bendera yataifa la Gabon Agosti 37, 2016 mjini Libreville.
Mfuasi wa kiongozi mkuu wa upinzani Jean Ping akishikilia bendera yataifa la Gabon Agosti 37, 2016 mjini Libreville. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wapatanishi wa Umoja wa Afrika walikua wakitarajiwa kuwasili mjini Libreville, mji mkuu wa Gabon, Ijumaa, Septemba 9, kujadili na wahusika wakuu wa mgogoro wa kisiasa nchini humo.

"Ujumbe huu umeahirishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu ya kalenda," amesema Bw Ngondet katika mkutano na waandishi wa habari.

Ujumbe wa wapatanishi ungeliongozwa na Rais wa Chad, Idriss Déby Itno, pia mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, na wenzake wa Congo - Brazzaville, Denis Sassou-Nguesso, Senegal, Macky Sall, kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa.

Maafisa wa Tume ya wa Umoja wa Afrika na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa wanaounda ujumbe huo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika aliahidi Jumatatu, Septemba 5, kushughulikia '' haraka utatuzi wa hali ya baada ya uchaguzi nchini Gabon kwa msaada wa nchi za ukanda ''.

Nchi hii inaendelea kukumbwa na mgogoro wa kisiasa ambao umesababisha vifo vya watu saba, baada ya Ali Bongo Ondimba kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Agosti 27.

Mpinzani Jean Ping, ambaye anabaini kwamba uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu, anapinga katu katu ushindi wa Ali Bongo Ondimba uliyotangazwa Agosti 31 na Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na tume ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.