Pata taarifa kuu
SUDAN

Khartoum kutangaza kumalizika kwa vita kwenye eneo la Darfur

Nchi ya Sudan, juma hili inatarajiwa kutangaza kumalizika kwa vita vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 13 kwenye jimbo la Darfur, licha ya mtanzuko uliojitokeza kwenye upatanishi uliokuwa unasimamiwa na umoja wa Afrika na kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano yaliyosababisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao.

Rais wa Sudan, Omar Bashir, akiwapungia wananchi wa taifa hilo hivi karibuni, atatangaza kumalizika kwa vita Darfur
Rais wa Sudan, Omar Bashir, akiwapungia wananchi wa taifa hilo hivi karibuni, atatangaza kumalizika kwa vita Darfur ibtimes.com
Matangazo ya kibiashara

Rais Omar Hassan al-Bashir, anatarajiwa kutoa tangazo hilo wakati wa sherehe zinazofanyika kaskazini mwa mji mkuu wa Darfur wa El Fasher, sherehe zinazotarajiwa kuhudhuriwa na Mfalme wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani pamoja na Rais wa Chad, Idriss Deby.

Nchi ya Qatar imekuwa mwenyeji wa mikutano kadhaa kati ya utawala wa kiislamu wa Khartoum na jamii ya makabila yenye watu wachache nchini humo, ambao walichukua silaha na kuanza kupambana na Serikali mwaka 2003.

Mazungumzo yaliyofanyika nchini Qatar mwaka 2011 yalipelekea kusainiwa kwa mkataba wa amani na kundi moja dogo la waasi la Liberation and Justice Movement, na Sherehe za Jumatano ya Agosti 7, zinaweka ishara ya utekelezwaji wa mkataba huo.

Wapiganaji wanaoisadia Serikali kwenye eneo la Darfur
Wapiganaji wanaoisadia Serikali kwenye eneo la Darfur AFP/Ashraf Shazly

Kituo cha televisheni cha taifa nchini Sudan, kimemnukuu gavana wa jimbo la Darfur Kaskazini, Abdelwahid Youssef, akisema kuwa Rais Bashir amehudhuria sherehe hizo na atatangaza rasmi kuwa makubaliano ya Doha kuhusu amani ya Darfur yametekelezwa kikamilifu.

Picha za televisheni zimewaonesha maelfu ya raia waliohudhuria sherehe hizo, huku wengi wakiwa na mabango yenye picha za Rais Bashir na mfalme wa Qatar.

Utawala wa Khartoum mara kadhaa ulitaka kutangaza kumalizika kwa vita kwenye eneo hilo toka mwanzoni mwa mwaka huu, ikidai kuwa kura ya maoni iliyofanyika mwezi April mwaka huu, iliungwa mkono na majimbo matano kwenye eneo hilo.

Lakini kura hiyo ambayo ilisusiwa na makundi ya waasi, ilikosolewa kwa sehemu kubwa na jumuiya ya kimataifa na mwezi Juni mwaka huu baraza la usalama la umoja wa Mataifa lilipiga kura kuongeza muda wa kusalia kwa tume yake ya kulinda amani kwenye jimbo la Darfur wanaoshirikiana na wale wa umoja wa Afrika.

REUTERS/Albert Gonzalez Farran/ys

Wanajeshi elfu 18 wanatarajiwa kusalia kwenye jimbo la Darfur, mpango ambao ulipingwa vikali na Serikali ya Khartoum.

Makundi mawili ya waasi kwenye eneo hilo, wale wa JEM na Sudan Liberation Army linaloongozwa na Minni Minnawi, walitia saini mapendekezo ya umoja wa Afrika kusitisha mapigano lakini mazungumzo kuhusu utekelezwaji wa mkataba huo yalivunjika mwezi uliopita.

Kundi la tatu la waasi la SLA linaloongozwa na Abdelwahid Nur bado halijatia saini mapendekezo hayo ya umoja wa Afrika, huku kundi la JEM lenyewe likisema litawaachia huru wafungwa wote inaowashikilia tangu kipindi cah mapigano dhidi ya Serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.