Pata taarifa kuu
GABON

Wananchi wa Gabon waendelea kusubiri kutangazwa kwa matokeo rasmi

Macho na masikio ya wananchi wa Gabon na Jumuiya ya Kimataifa, sasa yameelekezwa kwa tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo, CENAP, wakishinikiza tume hiyo imtangaze mshindi wa uchaguz mkuu uliofanyika mwishoni mwa juma, huku mchuano ukitarajiwa kuwa kati ya Rais Alo Bongo Ondimba na mpinzani wake mkuu Jean Ping.

Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba (Kushoto) na mpinzani wake Jean Ping (Kulia)
Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba (Kushoto) na mpinzani wake Jean Ping (Kulia) RFI/Montage
Matangazo ya kibiashara

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yalikuwa yatangazwe hapo jana kama ilivyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi, lakini hadi sasa utaratibu wa kutangazwa kwa matokeo hayo haujaanza, huku waandishi wa habari wa ndani na wale wa kimataifa wakiwa hawajaruhusiwa kuingia kwenye ukumbi wa kutangazia matokeo ambako kuna ulinzi mkali wa Polisi na wanajeshi.

Kwa mujibu wa sheria, waziri wa mambo ya ndani ya nchi anatakiwa kwenda kwenye ofisi za tume ya uchaguzi kutangaza matokeo rasmi baada ya kukamilika kwa zoezi la uhesabuji na ujumuishaji wa matokeo.

Kwa mujibu wa taarifa za kutoka ndani ya tume hiyo, kumekuwa na mjadala mkali kuhusu baadhi ya matokeo yaliyowasilishwa kwa tume hiyo, huku majimbo 8 kutoka kaskazini mwa nchi ambayo ni ngome kubwa ya vinara wanaowania Urais.

Ikiwa Ali Bongo anataka kushinda kinyang’anyiro hichi anatakiwa kupata zaidi ya kura elfu 60 kutoka kwenye jimbo la kaskazini la Ogooue, ambako waliopiga kura kwa mujibu wa tume walikuwa zaidi ya asilimia 90.

Toka mwishoni mwa juma mara baada ya kutamatika kuhesabiwa kwa kura kwenye maeneo mengi ya nchi, kiongozi wa upinzani Jean Ping, alijitangaza mshindi wa uchaguzi huo, kauli aliyoisisitiza hata jana na kumtaka Rais Bongo kukubali matokeo, akionya uchelewashwaji wa matokeo ya mwisho na tume ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.