Pata taarifa kuu
TANZANIA

Serikali ya Tanzania kuhamia Dodoma, wananchi wajiandaa kwa mabadiliko

Wakati waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, akijiandaa kuhamia mkoani Dodoma katikati mwa nchi ya Tanzania, wananchi wa mkoa huo wameitaka Serikali kuhakikisha inaboresha mazingira ya mji huo na kujiweka tayari kupokea ugeni mkubwa wa wafanyakazi wa Serikali.

Sehemu ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililoko mjini Dodoma Tanzania ambako Serikali inahamia.
Sehemu ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililoko mjini Dodoma Tanzania ambako Serikali inahamia. Ikulu/Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wetu aliyeko mjini Dodoma, Martha Saranga, ameshuhudia mabadiliko makubwa kwenye mkoa huo ambao sasa Serikali ya awamu ya tano inataka kuhamia huko kama ahadi yake ya kuhakikisha mkoa huo unakuwa makao makuu ya Serikali na nchi kama ilivyoasisiwa na marehemu baba wa taifa la Tanzania, Julius Kambarage Nyerere.

Harakati za kuhamia mkoani Dodoma hazikuanzia kwa Serikali ya wamu ya tano inayoongozwa na John Pombe Magufuli, lakini zilianza katika miaka ya 70, ambapo Rais wa kwanza Julius Nyerere, muasisi wa taifa hilo, alianzisha mchakato na kutangaza mkoa wa Dodoma kama makao makuu ya nchi.

http://michuzi-matukio.blogspot.com

Toka alipoondoka madarakani marais wote waliopita, Rais wa awamu ya pili Al-haji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na aliyemfuata Jakaya Kikwete, hawakufanikiwa kuanza mchakato wa kuhamia Dodoma.

Kwenye kampeni zake, kabla ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Rais Magufuli, aliwaahidi wananchi kuwa akiingia madarakani atahakikisha ndoto na mchakato ulioanzishwa na waasisi wa taifa hili, unatekelezwa, huku yeye mwenyewe akiahidi moaka kufikia mwaka 2020 Serikali yake yote itakuwa imehamia mkoani Dodoma.

Mwandishi wetu aliyeko Dodoma, anasema mji wa Dodoma umebadilika na wakazi wengi wengi wa mkoa huo wanaonekana kufurahia hatua ya Serikali kuanza kuhamia kwenye mkoa wao, wakisema toka tangazo la Serikali, kumekuwa na fursa nyingi za kiuchumi na kijamii.

Makutano ya barabara ya mwalimu Nyerere mjini Dodoma, Tanzania
Makutano ya barabara ya mwalimu Nyerere mjini Dodoma, Tanzania DR

Wenyeji wa mkoa huo licha ya kuunga mkono uamuzi wa Serikali, wanataka Serikali ihakikishe miundo mbinu ya mji huo inaboreshwa kikamilifu ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, huduma za afya, barabara, malazi na usalama.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Joram Rugimban, hivi karibuni akizungumza na idhaa hii, alisema kuwa mkoa wake uko tayari kuwapokea wafanyakazi wa Serikali, na kwamba zaidi ya asilimia 75 ya wafanyakazi hao wanauwezo wa kupatiwa makazi ya kuishi.

Haya yanajiri wakati huu waziri mkuu Kassim Majaliwa akitarajiwa kuwa kiongozi wa kwanza kuhamia mkoani Dodoma, ambapo anatarajiwa huko Alhamisi ya wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.