Mvutano nchini Zimbabwe: Mgomo mpya Jumatano hii
Nchini Zimbabwe, mvutano unaendelea kushuhudiwa wakati ambapo mgomo mpya unatarajiwa kufanyika Jumatano hii katika mji mkuu, Harare. Vyama vya kiraia vimewataka wananchi wa Zimbabwe kubakia nyumbani katika maandamano dhidi ya serikali ya Rais Robert Mugabe.
Imechapishwa:
Ni miezi kadhaa sasa maandamnao yakiendelea kushuhudiwa nchini humo.
Mashirika yote ya kiraia nchini Zimbabwe yamewataka raia kusalia makwao. "Wazimbabwe hawawezi tena," alisema Mchungaji Evan Mawarire, mmoj awa waandaaji wa mgomo huo. Ni lazima kutuma ujumbe kwa serikali, ameongeza, Mchungaji Mawarire, katika videoiliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii.
"Serikali hii inaendelea kutupiga, kutuweka jela, wakati ambapo hakuna kosa tunalofanya, tunaandamana kwa amani. Tunaheshimu sheria, kwa hiyo Serikali iache kuivunja kwa kutushambulia. Pia, Wazimbabwe, tunawatolea wito wa kudumisha umoja. Serikali hii inapaswa kuelewa kwamba tumechoka kwa namna tunavyohudumiwa. Tuna mawazo ya kuendeleza nchi hii, lakini hawataki kutusikiliza. "
Wote wanadai kujiuzulu kwa Robert Mugabe, ambaye yuko madarakani kwa miaka 36 sasa, na wanamshtumu kwamba anahusika kwa kuanguka kwa uchumi wa nchi. Kiwango cha ukosefu wa ajira kinakadiriwa kuwa zaidi ya 80% na nchi, hata hivyo, nchini sarafu za kitaifa na inakabiliwa na mfumuko wa bei.
Vuguvugu la Tajamuka, ikimaanisha "Tunahangaika," limeahidikuingia mitaani kila wiki hadi kuondoka kwa Rais Robert Mugabe.