Pata taarifa kuu
UN-BURUNDI

Mamia ya watu hawajulikani walipo, wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya watu waliopotea

Wakati dunia hii leo ikiadhimisha siku ya kimataifa ya watu waliotoweka, nchini Burundi kunaripotiwa matukio kadha wa kadha ya watu kuendelea kupotea katika mazingira ya kutatanisha huku vyombo vya usalama vikihusishwa.

Mmoja wa waandamanaji wakiwa wamevalia vitambaa kupinga kupotea kwa watu katika maandano yaliyofanyika hivi karibuni
Mmoja wa waandamanaji wakiwa wamevalia vitambaa kupinga kupotea kwa watu katika maandano yaliyofanyika hivi karibuni DR
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati wa haki za binadamu duniani wanakosoa baadhi ya Serikali barani Afrika kwa kutotilia maanani ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na vikosi vya nchi zao ambapo wamekuwa wakiwakamata watu na wasionekane tena.

Hivi karibuni shirika la kimataifa la Human Right Watch liliituhumu Serikali ya Kenya kwa kufumbia macho madai ya kuendelea kutoweka katika mazingira ya kutatanisha huku hakuna hatua ambazo zimechukuliwa kuwasaka watu hao.

Vitendo hivi vimeripotiwa pia kwenye nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na hasa kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo, ambaki kumeripotia vitendo vingi vya utekaji nyara.

Umoja wa Mataifa unayataka mataifa duniani kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wanaohusika na utekaji nyara, pamoja na kutofumbia macho taarifa za watu kuchukuliwa na vyombo vya dola kwenye mazingira ya kutatanisha bila kutolewa kwa taarifa kwenye familia zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.