Pata taarifa kuu
DRC-ADF-USALAMA

ADF yapata pigo kubwa baada ya kugunduliwa kambi yao kuu

Kwa mara ya kwanza, vyombo vya habari vya kimataifa vimealikwa kwenda kuona kambi iliyokuwa inadhibitiwa na waasi wa ADF NALU kwenye umbali wa kilomita 30 kaskazini mwa mji wa Ben, mashaiki mwa DRC, ambako mahandaki makubwa yalikuwa yamechimbwa chini ya ardhi.

Askari wa DRC katika eneo ambapo waasi wa ADF wanaendesha mauaji na uharibifu mali na vitu.
Askari wa DRC katika eneo ambapo waasi wa ADF wanaendesha mauaji na uharibifu mali na vitu. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Hii ni moja ya mafanikio makubwa ya jeshi nchini humo kurejesha kambi ya "Garlic", moja ya ngome ya ADF kwa kushirikiana na askari wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa MONUSCO.

Jenerali Ahmed Rakib, mmoja wa majenerali wa jeshi la Umoja wa Mataifa nchini humo na aliyetembelea kambi hiyo amezungumzia ueledi uliotumika na waasi hao kwa kujichimbia mahandaki hayo.

Waasi hao wanaodaiwa kuwa wa kundi la waasi wa Uganda wa ADF walihusika na vitendo viovu mbalimbali, hususan kuchoma misitu, hasa msitu uliokua karibu na kambi yao kwa lengo la kkabiliana na mashambulizi ya helikopta za jeshi na ndegege zisio na rubani zai kikosi cha jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO).

"Unaona, nafasi hii ilio wazi, hapa ndipo walikua wakikaushia chakula chao, na na mambo yao mengine," amesema jenerali Phiri kutoka Maawi, Mkuu wa kikosi cha Umoja wa wa Mataifa katika mji wa Beni.

Kugunduliwa kwa kambi hii ni pigo kubwa kwa waasi wa ADF, na huenda kundi hili sasa limeanza kupoteza nguvu zake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.