Pata taarifa kuu
DRC

Mpasuko wajitokeza ndani ya Upinzani nchini DRC

Viongozi wanne wa vyma avinavyounda muungano wa Dynamique de l’opposition nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameondolewa katika muungano huo kwa kukubali kushiriki katika kamati ya maandalizi kwa ajili ya mazungumzo nchini humo.

Kiongozi wa upinzani nchini DRC, Vital Kamerhe ambaye ametengwa na muungano wa upinzani
Kiongozi wa upinzani nchini DRC, Vital Kamerhe ambaye ametengwa na muungano wa upinzani DR
Matangazo ya kibiashara

Vyama hivyo ni pamoja na UNC cha Vital Kamerhe, PK cha Jeannot Mwenze Kongolo, CRP cha Fidele Tingomayi na kile cha ADT cha José Makila.

Hatua hiyo inakuja baada ya muungano huo kubaini kuwa viongozi hao wamekiuka msimamo waliokuwa nao kushikiza wafungwa wote wa kisiasa waachiwe huru na kusitisha kesi zote zinazodaiwa kubambikizwa.

Katika hatua nyingine, siku mbili baada ya kuzinduliwa rasmi kwa kamati hiyo, muundo wake umekabiliwa na tatizo la uwakilishi wa vyama vya upinzani na asasi za kiraia.

Kamati hiyo imerejelea shughuli zake baada ya mapumziko ya saa 24, huku vyama vikuu vya upinzani ikiwa ni pamoja na UDPS na MLC vikiendele kususia hadi kieleweke.

Akizungumza na RFI mjini Kinshasa kiongozi wa chama cha “Congo na Biso Freddy Matungulu Mbuyamu, amesema kuwa baada ya hatua ya vyama kuamua kushiriki katika shughuli hiyo bila masharti, muungano sasa umekosa imani nao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.