Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Makundi ya wanasiasa wa Sudan Kusini watishia kuandaa mpango kuipindua Serikali

Makundi ya wanasiasa wenye silaha na wale wasio na silaha wanaopinga Serikali ya Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiirm wamekubaliana kumuondoa madarakani katika kile walichosema ni utawala wake wa kiimla.

Mwanajeshi wa Sudan Kusini kama anavyoonekana katika picha iliyopigwa January 18, 2016
Mwanajeshi wa Sudan Kusini kama anavyoonekana katika picha iliyopigwa January 18, 2016 AFP PHOTO/Charles LOMODONG
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umefikiwa baada ya kikao chao kilichofanyika jijini Nairobi nchinik Kenya na kuhudhuriwa na aliyekuwa waziri wa kilimo, Lam Akol na aliyekuwa waziri wa Elimu, Peter Adwok Nyaba.

Viongozi hao wamesema kuwa hali ya mambo nchini mwao sio ya kuridhisha na kwamba uhasama wa kikabila umezidi kuongezeka toka Rais Salva Kiir alipoingia madarakani akiungwa mkono na wafuasi wa kabila lake la Dinka.

Kwenye taarifa yao viongozi hao wamesema wamaekubaliana kimsingi kuanza harakati za kuipindua Serikali ya Rais Salva Kiir katika kile walichosema ni njia pekee iliyosalia ya kuleta ukombozi kwenye taifa hilo.

Wanasiasa hawa wamekutana wakatik huu wakuu wa Juba, wakinukuliwa wakidai kuwa wasingependa kumuona aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais Riek Machar anarejea mjini Juba, na kwamba wao wakok tayari kutekeleza mkataba wa amani uliotiwa saini na Rais Kiir.

Toka kuondoka kwa Machar mjini Juba, hali ya sintofahamu imeendelea kushuhudiwa wakati huu nchik hiyo ikishuhudia mgawanyiko mkubwa wa kisiasa kati ya makundi yanayomuunga mkono Rais Kiir na Machar.

Jumuiya ya kimataifa imeendelea kutoa wito kwa Serikali ya Sudan Kusini kutekeleza mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi Agosti mwaka jana, ambapo unazitaka pande hizo mbili kusitisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.