Pata taarifa kuu
BENI-DRCQ

Watu wawili wameuawa kwa kukatwa mapanga mashariki mwa DRC

Watu wawili wameuawa kwa kukatwa na mapanga mkoani Beni mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tukio ambalo ni mfululizo wa mauaji ya kiholela yanayodaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda, ADF.

Wanajeshi wa Serikali ya DRC, wakiwa kwenye misitu ya Beni mashariki mwa DRC kuwasaka wapiganaji wa waasi wa Uganda, ADF ambao wanatekeleza mauaji ya kiholela
Wanajeshi wa Serikali ya DRC, wakiwa kwenye misitu ya Beni mashariki mwa DRC kuwasaka wapiganaji wa waasi wa Uganda, ADF ambao wanatekeleza mauaji ya kiholela UN Photo/Sylvain Liechti
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa maofisa wa jeshi kutoka Beni, Luteni Hazukay Mak, amesema kuwa tukio hilo limetekelezwa kwenye mji wa Kiteya jirani kabisa na Oicha, ambapo watu wawili waliuawa kwa kukatwa na mapanga, watu watano walijeruhiwa, nyumba saba, baiskeli na piki piki kuchomwa moto.

Kwa mujibu wa Mak, watu hao waliuawa majira ya saa moja usiku siku ya Jumatatu, na kuongeza kuwa kikosi maalumu cha wanajeshi wa umoja wa Mataifa walioko Beni walifanikiwa kunusuru maisha ya watu waliokuwa hatarini kuuawa.

Mji wa Kiteya uko kusini mwa Oicha, mji mkuu wa Beni ambao uko umbali wa kilometa 20 kaskazini mwa mji wa Beni.

Mji wa Beni umekuwa ukishuhudia mashambulizi kama haya toka mwezi October mwaka 2014, ambapo kwa mujibu wa taarifa ya umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 700 wameshauawa.

Mauaji ya mwisho kwa mujibu wa umoja wa mataifa, watu wanaofikia 50 waliuawa usiku wa Agosti 13 na 14 katika mji wa Rwangoma kaskazini mwa wilaya ya Beni jirani kabisa na mbuga ya Virunga, mauaji ambayo yaliripotiwa kutekelezwa na wapiganaji wa ADF.

Kundi la kiislamu la ADF ambalo liko mashariki mwa DRC toka mwaka 1995, linavituhumu vikosi vya Serikali, MONUSCO na vikosi maalumu vya umoja wa Mataifa kwa kuhusika na mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.