Pata taarifa kuu
DRC-JOSEPH KABILA

Serikali ya DRC kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa

Serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo imejiapiza kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa wakiwemo wanasiasa mashuhuri waliokamatwa na kuzuiwa mwaka jana katika warsha ya utawala bora barani Afrika.

Vijana wa taasisi ya Vijana wanaotetea demokrasia katika kampeini « Free Lucha »,mjini GOMA Februari 22 2016.
Vijana wa taasisi ya Vijana wanaotetea demokrasia katika kampeini « Free Lucha »,mjini GOMA Februari 22 2016. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Fred Bauma,mwenye umri wa miaka 26,ni mwanaharakati wa demokrasia LUCHA yenye makao yake mjini Goma katika eneo la Mashariki mwa Congo jimboni Kivu Kaskazini na Makwambala, mwenye umri wa miaka 33,mwenyeji wa Kinshasa mtumishi katika shirika la kiraia lijulikano kama Filimbi ambalo liliandaa warsha hiyo ya utawala bora walitiwa nguvuni mnamo march 15 mwaka jana.

Majina yao yalikuwa miongoni mwa majina ishirini na nne ya wafungwa waliopaswa kuachiwa huru kwa dhamana kwa mujibu wa orodha iliyosainiwa na waziri wa sheria nchini DRC Alexis Thambwe Mwamba.

Wawili hao walikamatwa kufuatia tuhuma za kuanzisha vurugu dhidi ya utawala wa raisi Joseph Kabila, na kufungwa jijini Kinshasa.

Katika ziara ya raisi Kabila mjini Goma juma hili alikutana na wanaharakati wa LUCHA ambao waliitaka serikali kulegeza vikwazo dhidi ya shughuli za kisiasa nchini humo.
Raisi Kabila aliwaahidi majibu ndani ya masaa arobaini na nane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.